MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu
Foundation, utakaofanyika Jumanne ya Agosti 5, katika Ukumbi wa Vijana
Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa 10 za jioni
ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha kabla ya
kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana,
alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi
kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.
kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.
Alisema
kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga, kinaonyesha namna
gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa ajili ya
kufanikisha mipango ya kimaendeleo.
“Tanzania
imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo taasisi imemualika
Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na wageni
waalikwa kuitambulisha taasisi.
“Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa
wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation,
ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.
wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation,
ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.
Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo itaanikwa
katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.
katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.
0 Comments