Gari
ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likiwa eneo la Mwanyamala mapema leo
mchana,ambapo moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba nzima na mali
zilizokuwemo,ambazo thamani yake haikujulikana mapema,tukio hilo
limetokea maeneo ya Mwananyamala jirani na hospitali ya Mwananyamala.
Baadhi
ya watu wakishuhudia tukio la Moto lililotokea mapema leo mchana,ambapo
moto huo umeteketeza nyumba nzima na mali zilizokuwemo,ambazo thamani
yake mpaka Globu ya jamii inaondoka eneo la tukio haikufahamika.
Baadhi
ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto
kwenye moja ya chumba cha nyumba hiyo,Mashuhuda waliokuweo kwenye tukio
hilo wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyokuwa
imetokea kwenye moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo.
0 Comments