NAIBU WAZIRI WA MAJI, MAKALLA AWANASA WEZI WA MAJI DAR NA KUTANGAZA KUFILISI MALI ZAO.


Meneja Mkuu wa Kampuni ya ufyatuaji matofali ya Ujenzi Solutions, ya Kimara  kwa Msuguri, Dar es Salaam, Rahim Hamis na mfanyabiashara wa kampuni isiyo na jina, Credo Rajab (kulia) wakiwa chini ya uliznzi wa Polisi  huku wakiwa wamevishwa pingu baada Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla  kuamuru kuwakamata alipokagua viwanda vyao vya ufyatuaji na kugundulika  kuwa wanatumia maji isivyo halali kwa kujiunganishia kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar  ws Salaam (DAWASA).  Makalla ambaye  alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Matambo wa Maji wa  Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani , pia alifanya msako wa kushitukiza kwa kampuni hizo.



Askari wa FFU wakilinda doria katika kiwanda cha ufatuaji tofali cha Ujenzi Solutions, Kimara Dar es Salaam
Moja ya mabomba linalodaiwa kuunganishwa kiholela kwenye bomba kuu la Ruvu  Juu linaloleta maji  mjini na kampuni ya Ujenzi Solutions eneo la Kimara
Makalla akizungumza mbele ya Lori la Maji lililokamatwa likijazwa maji
yanayodaiwa kuwa ya Dawass, katika kiwanda cha matofali cha Ujenzi
Solutions.

Post a Comment

0 Comments