Mkurugenzi wa uendeshaji NSSF , Crecentius Magori akizungumza.
KLABU ya
yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba kwa ajili ya wachezaji wake na
Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .Akizungumza
jana katika mkutano maalum na wachezaji hao Mkurugenzi wa uendeshaji NSSF , Crecentius Magori amewaambia
wachezaji hao kijana mjanja mjini ni yule ambaye ana miliki nyumba ama ardhi
kuliko magari huku akiwahamasisha wachezaji wa Yanga kuchangamkia ununuzi wa
nyumba hizo ambazo ziko katika mradi wa makao mapya katika kijiji cha Dege
Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Sisi tuko
tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha
nyumba hizo ambazo zimejengwa kisasa zaidi hivyo ningependa kuwashauri pindi mnapopata fedha zenu za mikataba mkitoa
kiasi ili kuweza kuwa kati ya wamiliki wa nyumba hizo” alisema Magori.
“Endapo
utaweza kumudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8
taslimu na kulipa kwa miezi
mitatu mfululizo unapewa NSSF wanamupa funguo
na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi hadi kwa miaka 15 unakuwa
mmiliki halali wa nyumba hiyo”alisema Magori.
Aidha
aliongeza kwa kuwaambia wachezaji hao kwamba endapo utakufa ndugu anaweza
kurithi nyumba hiyo.
Huku
akiwasisitiza wachezaji ambao bado hawajajiunga na NSSF kufanya hivyo mara moja
ili waweze kujivunia matunda ya uchezaji wa mpira hapo baadaye.
Wakati
huohuo Katibu wa Yanga Beno Njovu aliwaambia waandishi wa habari
kwamba hayo ni mawazo ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ambaye alizungumza na
Mkurugenzi wa NSSF Ramadhan Dau ambapo wote kwa pamoja wameamua kuwawezesha
wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na mali zao za kudumu hadi uzeeni.
Wavhezaji wa timu ya Yanga wakisikiliza kwa makini.
0 Comments