Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE Bibi
Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako
pichani) kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna
Bulondo.
Umetolewa
mwito kwa Watanzania kuzichangamkia fursa mbalimbali za kibiashara,
zinazoletwa na Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,
DITF ambapo Maonyesho ya huu, yatajumuisha makampuni zaidi ya kimataifa
toka nchi yatashiriki.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania, TANTRADE, Bibi Jaqueline Mneney Maleko wakati akizungumzia
maandalizi ya Maonyesho ya 38 Kimataifa ya Dar es Salaam, kwa
waandishi wa Habari, ofisi za TANTRADE jijini Dar es Salaam jana.
Bibi
Maleko amesema, lengo kuu la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, ni
kufungua fursa za kibiashara, kama fursa za kutafuta wabia, fursa za
kutafuta wawekezaji, na fursa za kuona bidhaa za viwango vya kimataifa
ili wazalishaji wa bidhaa za Tanzania kujitahidi kufikia viwango hivyo
vya kimataifa badala mtindo uliopo sasa kwa watu kujitokeza kwa wingi
kuja, kununua tuu bidhaa..
Maonyesho
ya mwaka huu, yatashirikisha waonyeshaji bidhaa zaidi ya 1,200 kati
yake Wizara, Idara na Wakala za serikali zaidi ya 60, na makampuni
zaidi ya 400 ya kimataifa yamethibitisha kushiriki.
Bibi
Maleko amesema hii ni fursa nzuri kwa Watanzania na Makampuni ya
Kitanzania kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa zinazoambatana na
maonyesho ya kimataifa.
Kauli
Mbiu ya Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ni
ni Kuunganisha Uzalishaji wa Bidhaa na Masoko, ili kutoa fursa kwa
wazalishaji wa bidhaa za Tanzania, kupata fursa za masoko ili bidhaa
hizo ziweze kukidhi vigezo vya kimataifa hivyo kuziwezesha kuingia
kwenye masoko ya kimataifa.
Bibi
Maleko, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania na haswa
wazalishaji bidhaa za Tanzania, ili kuweza kuingia kwenye ushindani wa
masoko ya ndani nay a kimataifa, ni muhimu kwanza ukajua mahitaji ya
soko, ndipo uzalishe bidhaa zitakazo kwenda sambamba na mahitaji na
vigezo vya masoko.
Ameeleza
kama kawaida kutakuwa na banda maalum la Tanzania lenye bidhaa za ndani
zilizikidhi viwango vya kimataifa ili kuwahamasisha Watanzania kupenda
bidhaa za ndani kwa kupenda chako, jenga chako.
Pia
maonyesho ya mwaka huu tayahusisha maonyresho ya biashara za bidhaa za
ubunifu na vipaji, zikiwemo bidhaa za mavazi, sanaa za maonyesho na hata
zanaa za muziki, hivyo kutakuwemo wanamuzi wataoonyesha bidhaa zao za
muziki.
Bibi
Maleko ametoa wito kwa Watanzania wasio na ajira, kuzitumia fursa za
maonyesho hayo ili waweze kujiajiri. TANTRADE itafanya kazi ya
kuwajengea uwezo, wakiwemo watu wenye makundi maalum kama wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu, hivyo TANTRADE iko kwa ajili ya kuwashika
mkono, kuwanjengea uwezo, kuwatafutia mitaji, uwezo na kuwatafutia
masoko.
Bi
Maloke aliwataka washiriki wote wa maonyesho hayo kufanya maandalizi
mapema na kufikia tarehe 27 ya mwezi huu, mabanda yote lazima yawe
yamemalizika, ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyosimamia Taasisi
ya Maonyesho ya Kimataifa ya UFI.
0 Comments