Meneja
Mipango na Mikakati wa Howard G. Buffet Foundation Tanzania Chapter Bi. Ellen
Mutalemwa akitoa rai wakati wa hafla ya kukabidhi Helkopta moja ambayo ni kati
ya ahadi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Mfuko huo alipomtembelea Rais Kikwete
hivi karibuni. Helkopta hiyo imetolewa ili kusaidi juhudi za Serikali katika
kupambana na ujangali katika hifadhi za Taifa
Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark
Childress (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Helkopta
kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara
mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet
(hayupo pichani) kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyarandu.Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
akiteta jambo na Wawakilishi wa Bunge .katika
hafla ya makabidhiano ya msaada wa Helkopta kwa ajili kupambana na ujangili
nchini Mh. James Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
Maliasili na Mazingira (katikati) na Mhe. Mch. Peter Msigwa Waziri Kivuli wa
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii Dkt.Idd Mfunda (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa
Kampuni ya Helkopta Charter (EA) Ltd Bw. Peter Achammer wakitiliana saini
katika hati za makabidhiano ya Helkopta moja iliyotolewa kama msaada na Taasisi
ya Howard G. Buffet Foundation ya nchini Marekani.Wanaoshuhudia zoezi hilo ni
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (aliyesimama kushoto) na Balozi
wa Marekani hapa nchini Mark Childress
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amepanda Helkopta ambayo
alikabidhiwa kama msaada kutoka Mfuko wa Howard G. Buffet kwa ajili ya kusaidia
juhudi za Serikali katika kupambana na ujangili.
Picha na Frank Shija, WHVUM
0 Comments