JESHI
la polisi mkoa wa Iringa kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi
shirikishi limefanikiwa kukamata mali za wizi zilizokuwa
zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo zikiwa na thamani ya Tsh
milioni 100 pamoja na lori lenye thamani ya Tsh milioni 100 ambalo
liliteketezwa kwa moto kabla ya dereva na utingo wa lori hilo
kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi.
Imedaiwa
kuwa watu zaidi ya 6 wanashikiliwa na jeshi hilo la polisi
akiwemo dereva na utingo wake ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la
wizi huo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi May 31 ambapo askari wa doria wilaya ya Mufindi
wakiwa katika shughuli hiyo ya doria walifanikiwa kuliona lori
hilo likiwa limeegeshwa kando ya barabara ya Iringa –Mbeya eneo la
Kinegembasi wilaya ya Mufindi huku likiwa limeteketea kwa moto katika
kibini yake.
Alisema
kuwa watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili T527 DPQ
likiwa na tela lenye namba T 974 EFE aina ya scania mali ya kampuni
ya Dandu ambalo walilikuta likiungua huku silizi zake zikiwa
zimefunguliwa na baada ya uchungu wa awali walibaini kuwa lori hilo
lilikuwa limebeba mitumba na viatu na baada ya msako ndipo
walipofanikiwa kukuta mitumba hiyo ikiwa imefichwa katika nyumba
moja kuukuu mali ya mama Gray Mpinga mwenyeji wa Maguhani Mufindi.
|
0 Comments