Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi
(aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi
wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa
wasichana uliofanyika Nigeria.
Mkurugenzi
wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa
kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini
Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.
Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea
mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa
na wanamgambo wa Boko Haram
Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga
vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.
Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi
wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya
kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa
wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanafunzi wakiwa na huzuni kwenye maandamano hayo.
Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi
wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya
kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa
wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram. Mkurugenzi wa WLAC, Theodosia Muhulo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika mkutano na
wanahabari
mara baada ya maandamano ya Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs)
na wanaharakati wengine kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana
uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.
MTANDAO
Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) nchini Tanzania pamoja na
baadhi ya wanafunzi wa kike shule kadhaa za Sekondari jijini Dar es
Salaam umefanya maandamano kupinga kitendo cha kikatili kilichofanywa na
kikundi cha Boko Haram cha nchini Nigeri cha kuwateka wanafunzi wa kike
na kuwashikilia.
Maandamano
hayo ya ndani yaliyoshirikisha wanaharakati mbalimbali yamefanyika
ndani ya viwanja vya TGNP Mtandao eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam,
ambapo viongozi wa mashirika yanayounda CSOs walipokea maandamano na
kusoma barua maalumu yenye ujumbe wa kupinga utekaji uliofanyika na
kuishinikiza Serikali ya Nigeria itekeleze matakwa ya watekaji ili
wanafunzi waliotekwa waachiwe huru.
Akisoma
barua hiyo kwa niaba ya CSOs, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP
Mtandao, Bi. Lilian Liundi alisema mashirika yao yanaotetea haki za
wanawake na watoto yameamua kuungana na mitandao na wanaharakati wengine
duniani kote kulaani kitendo cha kinyama cha kuwateka nyara wasichana
wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa shuleni nchini Nigeria, tukio
lililofanywa na wanamgambo wa kikundi cha Boko Haram.
"...Kwa
pamoja tunakitaka kikundi cha Boko Haram kuwaachia mara moja watoto hao
na kuwarudisha haraka majumbani kwao! Kama wanaharakati na watetezi wa
haki za wanawake na wasichana tunaitaka serikali ya Nigeria kuchukua
hatua zote muhimu zinazotakiwa ili kuokoa maisha ya wasichana hao wasio
na hatia, na
kuwahakikishia haki yao ya msingi ya kupata elimu na kutembea kwa uhuru bila vitisho," alisema Bi. Liundi.
Alisema
mashirika hayo yametumia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia
ulimwenguni kulaani kitendo hicho cha kikatili na kuitaka Serikali ya
Nigeria kuhakikisha inawajibikaji ipasavyo ili kuwarejesha mateka hao
mara moja tena wakiwa salama.
"Tunaikumbusha
serikali ya Nigeria kuzingatia na kutekeleza tamko la Umoja wa Mataifa
la haki za watoto (United Nations Convention on the Rights of the Child
(CRC) ambalo liliridhiwa na Tanzania mwaka 1989 na Nigeria mwaka 2003.
Mwisho tunatoa wito kwa viongozi wote wa Afrika na jumuia ya kimataifa
kuimarisha ulinzi wa wanawake na watoto ili kuhakikisha tukio kama hili
halitokei tena mahali pengine," alisema Liundi akisoma barua maalumu
itakayowasilishwa ubalozi wa Nigeria.
CSOs
wamelazimika kufanya maandamano hayo ya ndani baada yale ya kutaka
kuandamana hadi Ubalozi wa Nigeria kuzuiwa na Jeshi la Polisi kwa sababu
kadhaa. Hata hivyo baadhi ya askari polisi walikuwa pembeni mwa viwanja
vya TGNP Mtandao katika huku zoezi la maandamano ya ndani likiendelea.
Baadhi ya Mashirika yanayounda CSOs ni pamoja na TAMWA, TGNP Mtandao,
WiLDAF, LHRC.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
0 Comments