Social Icons

Tuesday, May 27, 2014

MGOMO WA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA JIJINI DAR



 Kamanda wa Polisi Kinondoni akiongea na waandishi wa habari kuelezea ni jinsi gani watashughulikia shida ya barabara hiyo ya kutoka kituoni makumbusho kuelekea mwenge
 Kondakta wa Daladala akiwa ameumia mkono wake wa kulia baada ya kukatwa na side mirror ya basi la UDA alipokuwa akilizuia lisipakie abiria na kuondoka kwenda mwenge
 Hapo ni Madereva na makondakta wakilikimbiza basi la UDA ambalo lilimkata mkono dereva mwenzao wakati wanalizuia lisiweze kutoka ndani ya kituo kuendelea na safari.
 Hili ni moja ya basi la abiria likiwa limewekea magogo ili lisiweze kuendelea na safari kuelekea mwenge Bali kuishia kituo cha makumbusho na kuweza kushiriki mgomo huo
 Daladala zikiwa zimepaki na kugoma kuendelea na safari ya kuelekea Mwenge
 
  Daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho zimepaki baada ya mgomo wao wa leo mchana
 Msururu wa daladala zikiwa ndani ya kituo cha makumbusho baada ya kugoma leo kuelekea mwenge kupeleka abiria
 Polisi wakiwa ndani ya kituo cha makumbusho kulinda usalama wa eneo hilo la kituo
 Daladala zikiwa zimepaki na kugomakupeleka abiria mwenge
Madereva na Makondakta wakizuia magari mengine kupita na kupeleka abiria
 Waandishi wa Habari wakichukua Maelezo kutoka kwa Afisa wa Polisi Kinondoni kuhusu mgomo huo wa daladala uliofanywa leo mchana na madereva wa magari ya Tandika,Mbagala,Buguruni ambayo yanatumia kituo cha Makumbusho kushusha abiria
 Madereva wa daladala kwa mbaliiii kama wanavyoonekana wakiendelea kuongea na Viongozi wa Serikali kuhusu Tatizo lao la barabara mbovu ya makumbusho kuelekea mwenge
 Madereva na Makondakta wa mabasi yanayofanya Safari zake kati ya mbagala,tandika kupitia kituo cha makumbusho wakijadiliana na viongozi wa sumatra na polisi  Ili kuweza kujua watatoa Suluhisho gani ili kuweza kutatua tatizo la barabara mbovu eneo la makumbusho
 
 Mkaguzi kutoka Sumatra akiongea na Vyombo vya habari na madereva na makondakta
 Afisa wa Polisi Kinondoni akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari baada ya kuweza kukubaliana na Madereva na Makondakta kutumia barabara kuu kwa siku mbili ili wakati wakiendelea kushughulikia utaratibu wa kutengenezwa kwa barabara za ndani ambazo walikuwa wanapaswa kuzitumia

No comments:

 
 
Blogger Templates