Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (kulia) akizungumza na wanafunzi wa Kike wa chuo cha CBE kampasi ya Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo la kuwakomboa kielimu.
Baadhi
ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho wakifurahia matukio mbalimbali
yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla ya uzinduzi wa mchakato wa
kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kike chuoni hapo wenye lengo
la kuwakomboa kielimu, kisiasa na kiutamaduni leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi
wa Kike wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya
pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya
Viwanda na Biashara Dkt. Mary Mwangisa (katikati). Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
======== ======== =========
WANAFUNZI WANAWAKE CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA DAR WAWEKA HISTORIA, WAANZISHA MFUKO WA KUWAKOMBOA KIELIMU.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
22/3/2014. Dar es salaam.
Wanafunzi
wanawake wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wamezindua
mchakato wa kuanzisha mfuko wa Jumuiya ya wanafunzi wa kike wenye lengo
la kumkomboa na kumwezesha mwanafunzi wa kike kujitambua, kielimu,
kisiasa na kiutamaduni.
Akizungumza
na jumuiya ya wanafunzi wa kike wa chuo hicho wakati wa uzinduzi wa
mfuko huo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa
Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Mery Mwangisa ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika hafla hiyo amesema kuwa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni
ishara ya umoja na mshikamano wa wanafunzi wa kike chuoni hapo.
Amesema
kuanzishwa kwa mfuko huo kunatokana na kuongezeka kwa changamoto
mbalimbali zinazowakabili wanawake pia kukosekana kwa mifuko ya aina
hiyo katika taasisi nyingi za elimu ya juu hapa nchini.
Ameeleza
kuwa malengo ya mfuko huo ni kumwezesha mwanafunzi wa kike wa CBE
kujitambua kielimu, kisiasa na kiutamaduni na kuongeza kuwa
yamekuja wakati muafaka kufuatia mabadiliko yaliyopo sasa ya kiuchumi,
kisiasa, kijamii na kiutamaduni.
Amefafanua
kuwa mfuko huo ulioanzishwa katika chuo hicho ni fursa pekee ya
kuwawezesha wanafunzi wa kike kunufaika kwa kupata elimu bora bila
vikwazo.
“Napenda
kutumia fursa hii kuushukuru uongozi wa chuo hiki kwa kuonyesha njia ya
kuwajali wanawake na pia katika kuweka taratibu nzuri za kulinda
maadili, katika maisha yangu sijawahi kusikia chuo kikuu chochote
kimezindua jukwaa la wanawake lenye malengo mazuri kama yenu” Amesema
Dkt. Mwangisa.
0 Comments