MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,
Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la
Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi, akisindikizwa na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega wakifurahia jambo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Ridhiwani Kikwete akiwa ameambatana na washindani
wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno
pamoja na Imani Madega na wadau wengine akielekea kurejesha fomu.
Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia tukio la Urudishwaji fomu wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo.
=========== ======== ======
Ridhiwani arudisha fomu za Ubunge Chalinze.
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,
Ridhiwani Kikwete leo amerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la
Chalinze kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi.
Akisindikizwa
na washindani wake katika kura za maoni, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma,
Ramadhan Maneno pamoja na Imani Madega, Ridhiwani aliwashukuru wana CCM
na wakazi wa Chalinze kwa ujumla kwa kumuunga mkono.
Ridhiwani
pia ameahidi kushirikiana na wanachalinze katika kutekeleza yote
yaliyofanywa na wabunge waliotangulia lakini pia amewataka wakazi wa
Chalinze kupuuza hoja inayotolewa na mgombe wa Chadema inayodhihaki kuwa
yeye sio mkazi wa Chalinze. Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Chalinze kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey alinukuliwa akisema kuwa
Ridhwani hawezi kugombea Ubunge Chalinze kwa kuwa sio mkazi wa Jimbo
hilo.
Aliongeza
kuwa ili kuwahakikishia wakazi wa Chalinze maendeleo inatakiwa kwa
wagombea kutangaza sera zinazotekelezeka na kuacha kutoa kauli zenye nia
ya kuwapumbaza wakazi wa Chalinze.
Alisema
kuwa hatotaka kutumia muda wake kufanya kampeni za kiubabaishaji kuanza
kurumbana na kukejeli kwa kuwa amekuwa katika misingi mizuri ya
kisiasa. Alisema hajatokea chumbani kugombania Ubunge badala yake
amekuwa katika misingi ya kisiasa tangia mdogo na amechukua uamuzi wa
kuingia katika siasa kwa lengo la kusaidia wananchi.
Alisema
kuwa kero kubwa inayowakabili wakazi wa Chalinze ni kukosekana kwa maji
ya uhakika, kero ambayo kwa sasa inatatuliwa kwa kuanzishwa kwa mradi
wa maji ya uhakika. Aliongeza kuwa pia kuna tatizo kubwa la ukosefu wa huduma bora za afya uhakika za afya kwa wakazi wa eneo la Chalinze. "Najua awali
wakazi wa eneo la Chalinze walikuwa wachache sana na kwa sasa
kuna ongezeko kubwa la wakazi wa Chalinze hivyo hata mahitaji
nayo yanaongezeka"alisema Ridhwani.
Aliongeza
kuwa ongezeko hilo limepelekea kuongezeka kwa uhitaji wa huduma
mbalimbali kama hizo za kijamii na kuongeza kuwa akiwa Mbunge atatatua
kero hizo."Watu wanadhania kuwa mimi nimetokea
chumbani kuja kwenye siasa hapana yani tena hata sio kwa sababu ya kuwa
mimi ni mtoto wa Rais ndio nimeona ngoja nije kuuza sura huku sio, ila
ni kwa sababu nimekulia katika mazingira haya na ninaona kuwa ni wakati
wa kutatua kero za wakazi wenzangu wa huku"alisema Ridhiwani.
Kuhusiana
na tatizo la migogoro katika jimbo hilo alisema kuwa anaona kuwa analo
jukumu kubwa la kuendelea kushiriki katika kutatua kero zao ambazo CCM
kwa muda mrefu imekuwa ikifanya hivyo. Alisema kuwa
atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu ya wafugaji na wakulima.
atakuwa na haki ya kupata mikosi iwapo akipuuzia kutatua kero ya muda mrefu ya wafugaji na wakulima.
Ridhwani anatarajia kuzindua rasmi kampeni yake Jumamosi ijayo katika jimbo la Chalinze. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze unafanyika kufuatia kifo cha aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Said Bwamdogo.
0 Comments