Kocha wa Mwadui Shinyanga, Jamhuri Kihwelu 'Julio' akikaribia kuipandisha daraja timu hiyo |
TIMU ya Mwadui Shinyanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kupanda Ligi
Kuu baada ya kuinyuka Toto Africans nyumbani kwao Mwanza kwa bao 1-0.
Mwadui inayofundishwa na Jamhuri Kihwelu 'Julio' kwa ushindi huo wa ugenini imefikisha jumla ya pointi 28 na imesaliwa na mechi moja, huku Toto Africans ikipoteza matumaini ya kurejea katika ligi hiyo.
Hii inatokana na Stand Utd pia ya Shinyanga iliyopo nafasi ya pili kuibutua JKT Kanembwa nyumbani kwao mjini Kigoma kwa mabao 3-2 na kufikisha jumla ya pointi 26 na kuendelea kuibana Mwadui ambao wamekuwa na upinzani mkubwa baina yao.
Toto iliyopo nafasi ya tatu imebakia na pointi 21 ambapo hata kama itashinda mechi yao ya mwisho haitaweza kuwafikisha popote na kuziacha timu pinzani za Shinyanga, Mwadui na Stand zikisubiri kujua hatma ya mmoja wao kupanda Ligi Kuu msimu wa 2014-2015 siku ya Aprili 5 mwaka huu.
Tayari timu mbili za Polisi Moro na Ndanda Fc zimeshafuzu ligi ya msimu ujao baada ya kuongoza kwenye makundi yao ya A na B.

0 Comments