Benki
ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu
baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria mpya dhidi ya mapenzi
ya jinsia moja.
Sheria
iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na
inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wafadhili
wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark
na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja
badala ya serikali.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi
kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema
waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao
nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza
kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana
serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya
Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa
muda misaada yake kwa Uganda.
CHANZO NI BBC SWAHILI
0 Comments