Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie
Nsoka akizungumza na wahariri na waandishi wa habari (hawapo pichani)
leo Makao Makuu ya Ofisi hizo, Sinza Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie
Nsoka akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam. Sehemu ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwa katika mkutano huo
Sehemu ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia mada katika mkutano huo Mmoja wa wahariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Lilian Timbuka (wa kwanza kushoto) akichangia mada katika mkutano huo. Sehemu ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka
amevipongeza vyombo vya habari kwa kutoa ushirikiano wa uandishi wa
habari za ukatili wa kijinsia ambao umeonesha mafanikio kwa sasa
ukilinganisha na mwamko uliokuwepo miaka ya nyuma.
Bi.
Nsoka ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha
taarifa ya matokeo ya utafiti wa mradi wa GEWE II (Mpango wa kutokomeza
ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto) kwa
wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari nchini.
Alisema
kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2012 hadi Septemba 2013, jumla ya habari
499 ziliandikwa kwenye magazeti mbalimbali kupitia mradi wa GEWE, huku
habari 216 zikiandikwa kwenye miradi mingine ya taasisi hiyo hivyo
kufanya idadi ya habari zote kufikia 715 kwa mwaka.
Alisema
ongezeko hilo limeleta mafanikio kadhaa kwa jamii hivyo kuwaomba
waandishi wa habari waongeze juhudi za uandishi wa habari za ukatili wa
kijinsia ili kukomesha vitendo hivyo vinavyo endelea kuiathiri jamii.
"...Hali
inaonesha uchapishaji wa habari uliongezeka zaidi kwa vitendo vya
ukatili, ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2012 ambapo uchapishaji wa
habari katika magazeti ulikuwa na Idadi ya 350 kwa miradi yote ya
TAMWA," alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema
ongezeko hilo la uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia limeleta
mafanikio kwa kiasi fulani, kwani kwa sasa jamii imepata uelewa kuhusu
masuala ya ukatili wa kijinsia na waliokuwa wakinyanyasika sasa
wamejitokeza kuomba msaada zaidi.
"...TAMWA
imekua ikipokea simu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania watu wakiomba
msaada wa kutatuliwa matatizo yao. Kituo ha usuluhishi cha TAMWA
kimekua kikipokea watu wakisema wamepata habari baada ya kusoma au kuona
machapisho au tangazo kupitia luninga au kusikiliza redio...," alisema
Bi. Nsoka.
Aidha
alisema waandishi wa habari wa Dar es salaam na mikoa mingi sasa
wameweza kuandika na kutangaza habari mbalimbali za ukatili wa kijinsia
kwa ufasaha.
Akizungumzia
matokeo ya utafiti wa kihabari uliofanywa na TAMWA kwa kushirikiana na
waandishi wa habari, alisema utafiti ulibaini kuwa asiliamia 17 ya
wananchi hawana uelewa wa sheria za ukatili wa kijinsia, huku Mkoa wa
Lindi kupitia Wilaya ya Lindi Vijijini ikiongoza kwa kupata asilimia 12.
Alisema
utafiti huo uliowahoji jumla ya watu 2,300 pia ulibaini kuwa asilimia
47 za kesi huripotiwa katika Serikali za vijiji na asilimia 25
huripotiwa katika vituo vya polisi. Utafiti ulinesha kuwa wananchi
hawana majukwaa ya kukaa pamoja na kujadili changamoto zao ambapo ni
asilimia 13.5 ndiyo wanachama wa asasi za kijamii.
TAMWA
kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari kiliwatuma waandishi wa
habari kwenda katika Wilaya 10 za mradi na kufanya utafiti ambao
matokeo yake yalitolewa mwezi Julai 2013. Wilaya 10 za Tanzania Bara na
Visiwani, ni pamoja na Kinondoni, Ilala, Kisarawe, Mvomero, Ruangwa,
Lindi Vijijini, Newala, Wete, Unguja Mjini Magharibi na Unguja Kusini.
0 Comments