Miyeyusho ‘alia’ kuandamwa na madeni


Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
Dar es Salaam. Bondia Francis Miyeyusho amesema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano lake na Viktor Chernous wa Ukrane kumemuingiza katika deni na kocha wake.
Bondia huyo amebainisha hadi jana mchana tayari alikuwa ametumia Sh2 milioni kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo la uzani wa super bantam huku pambano likihirishwa zaidi ya mara mbili.
“Hadi sasa sijui kama pambano litakuwepo hiyo Jumamosi au la kwani nimekuwa nikijifua, lakini sijaambiwa chochote kuhusu kuwepo kwa pambano hilo,” alisema Miyeyusho.
Alisema kuahirishwa mara kwa mara kwa pambano hilo kumemuingiza katika gharama kubwa za maandalizi yake.
Hadi jana mchana Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBF) halikuwa limetoa kibari cha pambano hilo ambapo rais wa TPBF, Chatta Michael alisema wanasubiri agizo la Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kutoa kibari cha pambano hilo.
Kwa mujibu wa promota wa pambano hilo, Jay Msangi huenda pambano hilo likasogezwa tena mbele endapo hakutapatikana kwa mwafaka kati yake na BMT ambayo ilimpa sharti la kulipa madeni yote ambayo anadaiwa licha ya kueleza tayari ametimiza masharti hayo na BMT bado inaendelea na msimamo wa kumfungia.

Post a Comment

0 Comments