Hata hivyo kipa tegemeo na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Juma Kaseja akiwa ameachwa nje.
Kikosi hicho kilichotangazwa na TFF badala ya kocha mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen na kuashiria kupewa 'mkono wa kwaheri' kwa kocha huyo kutoka Denmark na kitakachoingia kambini Machi Mosi na kuondoka nchini Machi 3 kwenda kuivaa wenyeji wao ni pamoja na makipa watatu ambao ni Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam).
Wengine waliotajwa ni mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).
Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.
TFF imesema wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.
0 Comments