EXTRA BONGO K KUZINDUA 'Mtenda Akitendewa' DAR LIVE FEB 22



Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kimya cha muda mrefu sasa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' ya Extra Bongo Next Level Wazee wa 'Kimbembe' ipo tayari kwa ajili ya mashabiki wa muziki wa dansi kupata burudani ya kusikiliza mitupio ya sauti kama ya kundi la Wenge Musica ambapo inatarajiwa Februari 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa maraha Dar Live Mbagala jijiji Dar es Salaam.
Mtenda Akitendewa ni albamu ya nne kwa bendi hiyo iliyoasisiwa kwa mara kwanza mwaka 2003 ikiwa na waimbaji Ally Choki, Bashiri Uhadi, Bob Kissa, Richard Maarifa, Khalidi Chokoraa, Flora Moses, rapa Greyson Semsekwa, (solo) Bonzo Kwembe, Efraim Joshua,George Gama (besi) Rythm na kinanda Thabit Abdul drum (ngoma) zikipigwa na Imma Chokolate.
Albamu ya kwanza iliitwa '3x3' ambao ni wimbo uliokuwa kwenye albamu nyimbo nyingine ni 'Regina Zanzibar', 'Tuchunge Wazazi au Fikiri
Madinda', 'Nunu Milenium' 'Walimwengu Remix' na 'Odise'.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema albamu hiyo imekamilika kwa asilimia zote na mashabiki wataanza kuipata siku hiyo ukumbini
ambako kutakuwa na burudani ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' wakiongozwa na Amin na Lina Sanga.
Khadija Omar Kopa sambamba na kundi la Makirikiri wa Bongo.
Licha ya wasanii hao pia bendi ya Mashujaa Watoto wa mama 'Sakina' itapamba uzinduzi huo huku 'Malikia wa Mipasho'.
Aidha Choki alisema, Prince Muumin Mwinjuma 'Kocha Dunia' naye ni miongoni mwanamuziki watakaoupamba usiku wa Mtenda Akitendewa.
Extra Bongo ilitikisa anga ya muziki wa dansi wakati huo na kuwa tishio kwa bendi kama African Stars 'Twanga Pepeta', FM Academia, Tanzania One Theatre (TOT) na nyinginezo hasa pale ilipoibuka na albamu ya pili iliyoitwa 'Bullet Proof' ikiwa na nyimbo kama 'Double Double' na 'Regina Zanzibar' kabla ya kusambaratika mwaka 2004.

Post a Comment

0 Comments