UCHAGUZI
Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),
utafanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam kama ulivyopangwa
na Kamati ya Utendaji ya chama.
Hata
hivyo sekretarieti ya TASWA imekubaliana kusogeza mbele muda wa kulipia
ada kwa wanachama hadi Jumanne Februari 4 mwaka huu, badala ya Ijumaa
Januari 31, 2014 iliyokuwa imepangwa awali, lengo likiwa ni kuwezesha
wanachama wengi zaidi kulipia ada zao ili waweze kushiriki uchaguzi huo.
Wanachama
wote walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2007 ama 2010 au Mkutano Mkuu wa
mwaka 2012 wana sifa ya kushiriki uchaguzi huo wanachotakiwa kufanya ni
kulipia ada zao kuanzia mwaka 2011.
Malipo
yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara, 0658-123082 na hakuna
mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama kwa sasa mpaka baada
ya Uchaguzi Mkuu.
Nawasisitiza
wanachama kuhakikisha wanatumia vizuri muda uliobaki kwa kulipia ada
zao ili waweze kushiriki mkutano huo. Kamati ya Uchaguzi ya TASWA
inatarajiwa kukutana Jumatatu ijayo kuzungumzia mambo mbalimbali
yahusiyo uchaguzi huo.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
29/01/2014.
0 Comments