Mtangazaji
wa Kipindi cha Power Breakfast, Paul James (PJ), akikabidhi msaada wa pedi kwa
mmoja wa wakina mama walio katika wodi ya wazazi wa hospitali ya Temeke.
Mtangazaji
wa Jahazi, Ephraim Kibonde akimfariji mmoja wa akina mama katika wodi ya wazazi
katika hospitali ya Temeke.
Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akimhoji mmoja wa vijana ambao wameacha kutumia madawa kwa msaada wa kituo cha Keko Youth. Clouds FMBaadhi ya wafanyakazi wa Clouds FM wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliokuwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, baada ya kukabidhi misaada yao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akiwa amempakata mtoto, baada ya kutembelea hospitali ya Temeke na kukabidhi misaada ikiwa ni sehemu ya miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji
wa kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa Dr
Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali ya Temeke,
ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji
wa kipindi cha Club 10, Perfect Chrispin akikabidhi michango ya papo kwa papo
iliyotolewa na wafanyakazi wa Clouds FM kwa kituo cha mwanzilishi wa kituo cha
Keko Youth, Yohana Victor Haule. Mbele yao ni mashine ya kupaka rangi
iliyotolewa na Clouds FM kama msaada kwa kituo hicho.
Mwanzilishi
wa kituo cha Keko Youth, Yohana Haule akimkabidhi Meneja wa Vipindi wa Clouds,
Seba Maganga, ikiwa ni kama shukrani kwa kutembelea kituo chao.
Shughuli za kijamii na burudani zatawala
Dar es Salaam, January
1, 2014: Kituo cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM leo kimefikia kilele
cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa.
Maadhimisho hayo
ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji wa vipindi
tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka hii 14 pamoja na
wasikilizaji wao sehemu walipo.
Leo ikiwa ndio siku ya
kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea hospitali ya Temeke na kituo
cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya kulevya cha Keko Youth, ambapo
misaada mbalimbali imetolewa.
Wakiwa katika hospital
ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya hospitali katika wodi ya
wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa vitendea kazi ambavyo vitawezesha
vijana kujiajiri baada ya kumaliza matibabu.
Akizungumzia
maadhimisho hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,
Joseph Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee kwa Clouds FM
hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha mambo
mengi makubwa toka walipoanza.
‘Maadhimisho haya ya
miaka 14 kwa mwaka huu yana lengo moja kubwa, kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa
kutufikisha hapa tulipo, na ndio maana tumeanza kwa kuwapa misaada wanaohitaji,
halafu tunamalizia kwa burudani’’ alisema Kusaga.
Akielezea zaidi
mafanikio ya Clouds FM kwa kipindi cha miaka 14, Kusaga alisema redio
imefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi, imeongeza ubunifu lakini pia kumekuwa
na uboreshaji wa hali ya juu wa mitambo ya kutangazia pamoja na maudhui.
‘Kwa kipindi cha miaka
mitatu mfululizo tumefanikiwa kushinda tuzo ya Super Brand, na kwa mwaka huu
pekee radio imefanikiwa kuanza kusikika mikoa ya Njombe, Songea, Njombe,
Sumbawanga, Katavi na Geita, kupitia mitandao kwa wasikilizaji wetu nje ya nchi
lakini pia tumefanikiwa kufanya tamasha la Fiesta kwa mafanikio zaidi’ alisema
Kusaga.
Kusaga pia aligusia
mchango wa Clouds FM katika kuhamasisha maendeleo na uzalendo hapa nchini
akitoa mfano wa semina za Fursa ambazo zilifanikiwa kwenda nchi nzima
zikizungumza na vijana kuamka na kuchangamkia fursa katika sehemu wanazoishi.
‘Semina za Fursa
zimekuwa mfano mkubwa namna Clouds FM ilivoweza kutumia nguvu yake kama radio
inayosikilizwa zaidi katika kuchagiza maendeleo, na kwa hakika mafanikio ya
semina yamekuwa ni makubwa sana’ alisisitiza Kusaga.
Kusaga pia alitoa
shukrani za pekee kwa watanzania kwa kuinga mkono Clouds FM sio kwa kusikiliza
tu bali hata katika kuhudhuria matamasha na shughuli nyingize za Clouds.
Kilele cha maadhimisho
ya miaka 14 ya Clouds FM kitamalizika kwa burudani kubwa ambayo itafanyika
katika viwanja vya Mwembeyanga ambayo itajumuisha wasanii na watu wengine
maarufu.
‘Kumekuwa na mafanikio
makubwa katika redio yetu kwa kipindi cha miaka 14, na naomba niseme, bila
ninyi wasikilizaji wetu tusingeweza kufika hapa’ alimaliza Kusaga.
0 Comments