MAELFU
ya wakazi wa mkoa wa Iringa na baadhi ya viongozi wa vyama
vya siasa na Serikali wakiongozwa na Rais Dr Jakaya Kikwete
wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga
na waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa.
Huku
waziri mkuu Mizengo pinda katika salam zake za serikali akielezea
jinsi ambavyo Taifa lilivyopata pigo kubwa kufuatia kifo cha Dr
Mgimwa kutokana na mchango wake katika baraza la mawaziri.
Katika
mazishi hayo yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga jimbo la
Kalenga wananchi mbali mbali walionyesha kujipanga barabarani
kutoka Manispaa ya Iringa hadi kijijini kwake huku wakiupungia
mkono msafara wa rais Kikwete na baadhi yao wakilazimika kutumia
usafiri wa baiskeli na pikipiki kwenda katika mazishi hayo.
Akitoa
shukrani za familia kwa niaba ya familia mtoto wa marehemu Dr
Mgimwa Godfrey Mgimwa aliishukuru serikali kwa jinsi ambavyo
ilivyohangaika kumuuguza baba yake na kutoa wosia mzito wa marehemu
Dr Mgimwa ambao alimtaka kuufikisha kwa Rais Kikwete..
Alisema
katika uhai wake kabla ya kifo chake ikiwa ni siku tano kabla Dr
Mgimwa alimwita na kumtaka kufikisha shukrani zake kwa Rais
Kikwete kwa kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa
pamoja na spika wa bunge Anne makinda .
Pia
alisema kuwa alieleza dhamira yake ya kuwatumikia wana Kalenga na
kusema zawadi kubwa ni msaada wa bati zaidi ya 2000 kwa wananchi hao
ili kuendeleza ujenzi wa shule na vituo vya afya jimboni.
"Baba
kabla ya kufa aliniachia wosia huo juu ya wana Kalenga kwa
kuwashukuru kwa ushirikiano wao na kutoa bati ila alipenda kuona
Kalenga inakuwa na maendeleo zaidi"
Kwa
upande wake waziri Mkuu Pinda alisema kuwa serikali imepata pigo
kubwa juu ya kifo hicho na kuwa bado serikali itaendelea kuwa karibu
na familia ya Dr Mgimwa na pale penye tatizo isisite kuwasiliana .
Hata
hivyo Rais Kikwete hakupata kuzungumza chochote katika msiba
huo zaidi ya kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono
ndugu wa Dr Mgimwa .
Spika
wa bunge Anne Makinda alisema kuwa bunge limempoteza kiongozi na
mbunge aliyependa kutumia nafasi yake kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe
mchango wake hawataacha kuukumbuka.PICHA NA HABARI KWA HISANI YA
FRANSIS GODWIN IRINGA
|
0 Comments