MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji
JKT Ruvu na Coastal Union ya Tanga iliyochezwa juzi (Novemba 6 mwaka huu)
Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam imeingiza sh. 201,000.
JKT Ruvu iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi
hiyo namba 85 na kushuhudiwa na watazamaji 67 waliokata tiketi kwa viingilio
vya sh. 3,000 na 10,000.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 39,010 wakati Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 30,661.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 19,835, tiketi sh. 38,100, gharama za mechi sh. 11,901, Bodi ya Ligi
sh. 11,901, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,950 na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,628.
Nayo mechi kati ya Ashanti United na Simba iliyochezwa
juzi Uwanja wa Taifa imeingiza sh. 24,931,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo
wa sh. 5,333,590.
Wakati huo huo, mechi za jana (Novemba 7 mwaka huu) kati ya Yanga na Oljoro imeingiza sh. 34,902,000 kutokana na watazamaji 6,045 ambapo kila klabu imepata sh. 7,812,477.95. Mechi ya Azam na Mbeya City iliyochezwa Azam Complex yenyewe imeingiza sh. 15,973,000 kwa watazamaji 4,857 na kila klabu imepata sh. 3,953,162
0 Comments