Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi isiyoya
kiserikali ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMAF) Dkt. Ellen Senkoro
(kulia) akisisitiza jambo wakati wa makabidhiano ya msaada wa kiasi cha Sh.
milioni 50 za kitanzania mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa
BMAF. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita
Gold Mine (GGM) Balozi Richard Mariki.
Mkurugenzi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita
Gold Mine (GGM) Balozi Richard Mariki (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa
makabidhiano ya msaada wa kiasi cha Sh. milioni 50 za kitanzania mbele ya
waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa BMAF. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
mtendaji wa Taasisi isiyoya kiserikali ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMAF)
Dkt. Ellen Senkoro
Mkurugenzi wa Kampuni
ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine (GGM) Balozi Richard Mariki (kushoto)
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyoya kiserikali ya Benjamin
William Mkapa Foundation (BMAF) Dkt. Ellen Senkoro bahasha yenye nembo ya
kampuni GGM kama ishara ya kupokea msaada wa kiasi cha Sh. milioni 50 za
kitanzania mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa BMAF.Picha zote na
Lorietha Lawrence-Maelezo
(Eleuteri
Mangi-Maelezo)
Taasisi isiyoya
kiserikali ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMAF) imepokea msaada wa kiasi
cha Sh. milioni 50 za kitanzania kwa mwaka 2013 katika kutekeleza mpango
mkakati wake wa miaka mitano kwa awamu ya pili kati ya mwaka 2012 hadi 2017.
Makabidhiano hayo
yalifanyika hivi karibuni katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini
Dar es salaam kati ya Mkurugenzi mtendaji wa BMAF Dkt. Ellen Senkoro na Mkurugenzi
wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine (GGM) inayojishughulisha na
uchimbaji wa madini ya dhahabu Balozi Richard Mariki.
Dkt. Senkoro alisema kuwa msaada huo kwa
taasisis yake utatumika katika mradi wa kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa
upande wa ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS) na huduma kwa akinamama wajawazito na
watoto wachanga (MNH) kupitia mpango unaosimamia kuimarisha afya ya rasilimali watu
“Taasisi yetu
inaendelea na mpango wa kukusanya rasilimali kwa kuangalia malengo ya muda
mrefu kupitia marafiki na wahisani mbalimbali wakiwemo GGM na makampuni mengine
makubwa ndani na nje ya nchi.”alisema Dkt. Senkoro
Dkt. Senkoro alisema
kuwa BMAF katika kipindi hicho cha miaka mitano inatarajia kukusanya jumla ya
Sh. bilioni 12 za kitanzania ambapo lengo ni kukusanya Sh. bilioni tatu za
kitanzania kwa mwaka ili kuboresha huduma za afya katika wilaya 15 nchini.
Dkt. Senkoro alisema
kuwa lengo ni kufikisha huduma kwenye wilaya 15 nchini ambapo tayari wilaya
sita zimeanza kunufaika na mradi huo ambazo ni Kahama, Kishapu (mkoa wa
Shinyanga), Sumbawanga vijijini, Kalambo na Nkasi (mkoa wa Rukwa), na
Biharamulo (mikoa ya Kagera).
Wilaya nyingine
zitakazonufaika na huduma hiyo kwa awamu ya pili zipo tisa ambazo ni Shinyanga
vijijini, Meatu, Bariadi, Halmashsuri ya mji wa Sumbawanga,Maswa, Itilima,
Busega, Mkoa wa kati-Pemba, na Chake- Unguja vijijini.
Aidha, Dkt. Senkoro
alisema kuwa BMAF tayari imewaajiri watoa huduma 30 katika maeneo ya watabibu, manesi
na watoa huduma wasaididzi wa maabara ili kufanikisha na kuboresha utoaji
huduma na mradi huo kuwa endelevu.
Vivyo hivyo Dkt.
Senkoro alisema kuwa BMAF inawhudumu 32 tayari ambao wanatoa huduma katika
wilaya zilizoainishwa na itaendelea kuajiri wengine 30 katika Nyanja za kutoa
huduma kwa wagonjwa wa ukimwi, huduma ya haraka kwa akinamama wajawazito ambazo
ndizo nyenzo mahususi kwa kuokoa maisha ya akinamama hao wanapokuwa na matatizo
wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Geita Gold Mine (GGM)
inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu Balozi Richard Mariki
alisema kuwa wanafarijika kuona msaada wanaotoa unatumika kulingana na maelengo
yaliyokusudiwa.
Vivyo, Balozi Mariki
ameishukuru BMAF kwa kuchagua kushirikiana na GGM katika kutoa huduma kwa jamii
na ameahidi kuendelea kushirikiana nao kwani wote wanalenga kumhudumia mwananchi
mhitaji.
0 Comments