Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia na kusikiliza maelezo kuhusu maandalizi ya jinsi ya kukamua
mafuta ya Mawese kutoka kwa Meneja wa mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya
Ziwa Tanganyika, Seleboni John Mushi, wakati Makamu alipozindua mradi
huo jana Igalula, Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma. Dkt. Bilal,
alitembelea na kukagua mradi huo unaosimamiwa na Ofisi yake na kujionea
jinsi mafuta hayo yanavyopatikana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Vikundi
vidogo vya Uchakataji Mawese Igalula Mkoa wa Kigoma, wakati wa hafla
hiyo iliyofanyika jana Wilayani Uvinza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Makamu wa Rais, Sazi Salula. Mradi huo unasimamiwa na Ofisi ya Makamu
wa Rais.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kuhusu ukamuaji wa mafuta ya Mawese Kaimu Meneja wa
kutoka kwa Meneja Sido Mkoa wa Kigoma, Gervas Ntahamba, wakati wa hafla
ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika jana Igalula, Wilaya ya Uvinza
Mkoa wa Kigoma. Dkt. Bilal, alitembelea na kukagua mradi huo
unaosimamiwa na Ofisi yake na kujionea jinsi mafuta hayo
yanavyopatikana.Picha na OMR
0 Comments