Mgeni
rasmi katika mbio za Tabora Marathon 2013, Mkuu wa Wilaya ya Tabora
Mjini, Suleiman Kumchaya, akimkabidhi zawadi ya kitita cha sh 100,000
mshindi wa mbio za Kilomita 15, Grace Jackson.
Mgeni
rasmi katika mbio za Tabora Marathon 2013, Mkuu wa Wilaya ya Tabora
Mjini, Suleiman Kumchaya, akimvisha medali mshindi wa mbio za Kilomita
15.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
mkoani Tabora imepongeza mashindano ya Tabora Marathon kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa na kwamba itakuwa bega kwa bega katika mashindano yajayo
ya mwaka 2014.
Mkuu
wa Wilaya ya Tabora Mjini (DC), Suleiman Kumchaya, ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi kwenye mbio hizo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Fatma Mwassa, alitoa
pongezi hizo kwenye kilele cha mbio hizo zilizomalizikia kwenye viwanja
vya taasisi mjini hapa.
Kumchaya alisema, amefarijika sana kuona vijana,wazee na watoto wamejitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Tabora Marathon.
Hata
hivyo aliwashauri washiriki wote kuunda vikundi kwenye maeneo yao ili
wanapopata muda wanafanya mazoezi ya riadha na hata mashindano
yatakapokuja mwakani wanakuwa fiti kimwili.
Kumchaya aliwaasa viongozi wa riadha mkoa wa Tabora, RITAM kwa kushirikiana na Kamati ya Tabora Marathon, kuanza maandalizi
ya mbio za 2014,na baada ya kikao cha tathimini, wahakikishe wanakutana
naye ofisini kwake kuweka mambo sawa kwa mbio zijazo.
Katika
hatua nyingine serikali iliwapongeza wadau walijitokeza katika michango
yao,kuwa serikali itandaa barua za kuwatambua wote kama shukrani kwao.
Wafadhili
waliochangia kufanikisha mbio hizo ni Vodacom Tanzania, Filbert Bayi
Foundation, mwanariadha wa kike, Banuelia Brighton, Meneja mfuko wa
taifa wa bima ya afya Kanda ya Magharibi, Emmanuel Aidan, kampuni ya
Tumbaku, ATTT, Mkurugenzi wa GONALLA Phamacy, Godbless Mafole, Posta,
NMB, TRA NHC, MVP, Platnum Credit.
Tabora
Marathon 2013, ilishirikisha mbio za Nusu Marathon Kilomita 21 kwa
wanaume, Kilomita 15 kwa wanawake na Kilomita 5 kwa watoto na wazima.
Katika
kilomita 21, mshindi wa kwanza aliibuka Tabu Mwandu aliyetumia saa
1:10.35 aliyezawadiwa kitita cha sh 100,000, kikombe na medali ya
dhahabu, wa pili Dickson Mkami saa 1:13.18 na kujipatia sh 70,000 medali
ya fedha huku nafasi ya tatu ikienda kwa Francis Jombe aliyetumia saa
1:14.36 na kuzawadiwa sh 60,000 na medali ya shaba.
Aidha
kilomita 15 wanawake, Grace Jackson alishinda akitumia dakika 55:33.06
na kuzawadiwa sh 100,000, medali ya dhahabu na kikombe, wa pili Maombi
Elisha dakika 58:52.01 na kuzawadiwa sh 70,000 na medali ya fedha huku
nafasi ya tatu ikienda kwa Naomi Samweli aliyetumia saa 1:00.05
aliyejipoza kwa sh 60,000 na medaliya shaba.
Washindi
wa nne na tano kila upande walizawadiwa sh 20,000 kila mmoja huku wa
sita hadi wa kumi wakijipoza kwa sh 15,000 kila mmoja.
Kwa
kilomita 5 wanaume wa kwanza aliibuka Robert Mayala wa pili ni Joseph
Kimatile na kufuatiwa na Rashid Malugu waliopata medali za dhahabu,
fedha na shaba.
Upande
wa wanawake kilomita tano ni Getruda Musa wa pili Sara Lyimo na Asha
Seleman ambao nao walipata medali, huku mkimbiaji mwenye umri mkubwa
Msese Said (65), Msese Said akipata fedha sh 17,000 kutoka kwa akiwamo
DC Kumchaya.
0 Comments