UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BFT KUFANYIKA JULAI 7 MWAKA HUU



TANZANIA BOXING NEWS: UCHAGUZI BFT JULAI 7


Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.

Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika  ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi 
cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha  
kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani 
kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na 
kinyume na katiba yetu.

Upotoshaji huo unafanywa na  Akaroly Godfrey aliyekuwa  kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya 
na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha 
dunia (AIBA) na kusababisha  kutoshiriki mashindano,mikutano na 
shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba 
wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la 
masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga 
mbele.

Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini 
Mwanza na tarehe hiyo  ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na 
kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.

Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika 
uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, 
waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu 
ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013

BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu.

Post a Comment

0 Comments