UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
OFFICE OF THE DEPUTY VICE-CHANCELLOR
(ADMINISTRATION)
OFFICE OF THE DEPUTY VICE-CHANCELLOR
(ADMINISTRATION)
P.O. BOX 35091 - DAR ES SALAAM - TANZANIA
.
|
Tel.: 022 2410500 - 8 Ext.
2003
022 2410394 - Direct Line Fax: 022 2410718 Ref: z1/18 |
21 Juni,
2013
Wanajumuiya Wote
YAH: KUFUNGWA KWA SEHEMU YA BARABARA YA KONTENA—KANISANI/MSIKITINI— CHANGANYIKENI
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unautaarifu umma kuwa kipande cha barabara kuanzia kumbi za mihadhara ya Yombo 1&2 na Bweni Na. 6 hadi barabara ya Changanyikeni kitafungwa kuanzia Jumapili tarehe 23 Juni 2013.
Barabara inayoanzia kituo cha daladala cha Kontena hadi Bweni Na. 6 ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya Chuo tu, ingawa kwa siku za karibuni matumizi ya barabara hiyo yameongezeka kiasi cha kuhatarisha usalama wa wanafunzi na wafanyakazi wanaotumia kumbi za mihadhara na ofisi zilizopo maeneo hayo.
Kwa hiyo, watu wote waliozoea kutumia barabara hiyo kuelekea Changanyikeni kwa vyombo vya usafiri vya moto, wanashauriwa kutumia barabara ya kawaida inayoanzia au kutokea karibu na tawi la NBC.
Tunawapa pole kwa usumbufu utakaojitokeza kwa kufungwa kwa barabara hiyo.
Prof. Y. D. Mgaya
NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO - UTAWALA

0 Comments