Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa
Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini
hiyo iliyohusu na harakati
rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema
leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa
Dodoma.kutakuwepo
na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya
uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa. Aidha pia mchana
huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za
kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika
uwanja wa jamhuri .
Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Patrick Ngowi kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia
fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni
namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi
kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo.
Mmoja
wa washiriki wa semina hiyo akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwa kuhusiana
na mambo mbalimbali ya ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo
katika kujikwamua kimaisha.
Mh
Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa
akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna
ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo
watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia.
0 Comments