BAADA YA KUSUSA KULA SIKU2 SASA AFANDE MAMBO SAAFII


BAADA ya kususa kula kwa siku mbili mkali wa ghani ‘Rymes’ nchini msanii Selemani Msindi ‘Afande Sele’ amesema ameanza kula baada ya kushusha fundo lake la timu ya Simba kulala 2-0 na watani wao wa jadi Yanga.
Afande Sele ameweka wazi ilibidi agome kula kutokana na mke wake  ambaye ni shabiki wa  Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga.Msindi aligoma kula siku moja baada ya mechi hiyo ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyopigwa Mei 18 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza kwa njia ya simu  na Bongoweekend alisema kwamba uchungu ulizidi baada ya mkewake  mama Tunda alizidisha utani nyumbani kwake hivyo akaona bora asuse kula kwa siku mbili lakini sasa maisha yanaendelea ,huku akimalizia kwa kicheko.

Post a Comment

0 Comments