WATENDAJI WA SERIKALI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA WAASWA KUZINGATIA MAAGIZO KUTOKA CHAMA TAWALA ILI KUFANIKISHA SHUGHULI ZA UTENDAJI KAZI



  

 Na Elizabeth Ntambala, Sumbawanga

Watendaji wa serikali wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wametakiwa kuzingatia maagizo ya viongozi wa chama Tawala kwenye maeneo yao ya kazi badala ya kuyapuuzia na kufanya kazi kinyume na ilani ya uchaguzi wa chama hicho.

Wito huo unafuatia baadhi ya Watendaji wa serikali katika wilaya hiyo kuonekana kutofungamana na viongozi wa CCM  katika utendaji wa kazi zao huku wakidai kuwa wao sio wanachama wa chama chochote bali ni watendaji wanaotakiwa kufanya kai za serikali pekee.

Akizungumza katika mikutano tofauti aliyoifanya mwishoni mwa wiki ,kwenye kata ya Mtowisa na Milepa, Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Jimbo la Kwela Ignas Malocha alisema hivi sasa  yapo malalamiko ya viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali ambayo yanaelekeza lawama kwa baadhi ya watumishi wa serikali wanaokataa kufuatiliwa utendaji wao wa kazi na viongozi wa chama kinyume ilani ya chama hicho

“Kuanzia leo mfahamu kuwa nyie watumishi wa serikali ni sawa na wauza duka wa CCM, tumewaweka kwaajili ya kutekeleza ilani yetu , hivyo mnatakiwa kufuata maelekezo ya chama kilichopo madarakani  na  hii ni kwa chama kitakachopata fursa ya kuchukua madaraka iwe Chadema,CUF , NCCR na chama kingine chochote”.

Alisema kitendo cha watumishi wa serikali kukubali kusimamiwa utendaji wao wa kazi na viongozi wa chama tawala hakumaanishi kuwa wao ni wanachama wa CCM, bali ni wajibu wa viongozi wa CCM kuhakikisha kuwa ilani yao inatekelezwa na hakuna mtu yeyote atakayeingusha kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kushughulikia kero za wananchi pasipo kujali itikadi zao.

“Hapa kinachotakiwa ni kuona Mtanzania anapata huduma anayostahili ikiwa ni pamoja na matibabu, elimu, maji na mambo mengineyo ya msingi hivyo simamieni hayo , kwani tatizo la wananchi ni kutaka kuhudumiwa vizuri na serikali ya na  vitu na kuishi kwa amani”. Alisema.

Aidha alikemea tabia za baadhi ya Watendaji wa serikali kuwageuza wananchi kuwa migodi yao kwa kuwadai rushwa pale wanapokwenda kwenye ofisi zao kupata huduma.

Alisema..“Huku vijijini ukwaona baadhi ya  VEO na WEO ndio wafalme kwani wengi wao wamekuwa wakilaumiwa kwa vitendo vya rushwa vinavyotokana na migogoro ya ardhi, ugomvi baina ya wakulima na wafugaji ”.

“Jamani waacheni hawa wananchi waishi wa kufaidi nchi yao na sio kuwakera kwa mambo kama haya , nataka ni wahakikishie hata kama siku CCM itaondoka madarakani hakuna kiongozi yeyote wa chama kingine kitakachochukua  madaraka ambaye atafanya sherehe kwa wapiga kura wake kunyanyasika”. Alisema Malocha.

Post a Comment

0 Comments