KATIKA hali isiyo ya kawaida waya wenye thamani ya zaidi ya Tsh300Millioni
mali ya Serikali ya mapinduzi Zanzibar umeuzwa kwa Tsh.2.5Millioni na baadhi ya
maafisa wa serikali hiyo hali iliyosababisha makamu wa pili wa Rais Zanzibar
kuzuia uuzwaji wa waya huo na kampuni iliyonunua.
Tukio
hilo limebainika mara baada ya Makamu huyo kutembelea kwenye kiwanda Cha Sukari
kilichopo Mahonda mjini Zanzibar na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho,
ambacho kiliuziwa waya huo kwa bei chee.
Balozi
Seif alisema zipo hitilafu zinazotumiwa na baadhi ya maafisa wa Serikali katika
mauzo ya mali za Serikali na matokeo yake kusababisha kuitia hasara kubwa
Serikali Kuu.
Amesema
Mali za Serikali zimekuwa zikinunuliwa kwa gharama kubwa lakini uuzwaji wake
baada ya matumizi hayalingani na thamani ya mali zenyewe jambo ambalo hutoa
mwanya kwa mali hizo kuuzwa kwa bei ya chini kabisa.
“
Utashangaa kuona mali za Serikali hununuliwa kwa gharama kubwa lakini baadhi ya
maafisa na watendaji wa serikali hutumia mwanya wa kujenga hoja ya kuuzwa mali
hizo kwa kisingizio cha kuchakaa na badala yake baadhi yao kujiuzia wenyewe kwa
bei wanayoitaka wao wenyewe bila ya kuzingatia taratibu zilizopo za tenda na
mnada”. Alionya Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuagiza Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais
Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kukaa pamoja na Uongozi wa Kiwanda cha
Sukari kuangalia nanma ya matumizi ya
waya huo ambao ulikuwa ukitumiwa na Kiwanda hicho.
Waya
huo ulilazimika kufukuliwa na Uongozi wa Kiwanda hicho baada ya kubainika
kuanza kuhujumiwa kwa kukatwa katwa na baadhi ya wezi kufuatia kutambulikana
thamani yake katika masoko ya Kimataifa.
Mapema Mshauri wa Kiwanda cha Sukari
Mahonda Dr. Hamza Hussein Sabri alisema
Zanzibar inatarajiwa kujitosheleza kwa Sukari ifikapo mwishoni mwa mwezi Oktoba
mwaka huu kufuatia uongozi wa Kiwanda cha sukari Mahonda kufanikiwa kupata
washirika zaidi katika kuongeza nguvu ya kuanza uzalishaji wa bidhaa hiyo
muhimu kwa matumizi ya Jamii.
0 Comments