Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa timu ya Azam ya
Tanzania Bara kwa kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la
Shirikisho iliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Ushindi
wa jumla ya mabao 8-1 ambao Azam imeupata dhidi ya Al Nasir Juba ya
Sudan Kusini si fahari kwa timu hiyo tu, bali Tanzania kwa ujumla, na
unaonyesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kiushindani katika michuano
hiyo ya Afrika.
Hata
hivyo, ni vizuri Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na
wachezaji wa timu hiyo wakautazama ushindi huo kama changamoto kwao
kuhakikisha wanajipanga vizuri zaidi kwa raundi inayofuata.
Timu
ya Azam inayofundishwa na Mwingereza John Stewart Hall ilishinda
nyumbani mechi ya kwanza mabao 3-1, na jana kuibuka na ushindi wa mabao
5-0 ugenini jijini Juba.
Kwa
kufanikiwa kuing’oa Al Nasir Juba, Azam sasa watacheza raundi ya kwanza
(raundi ya 16 bora) ya michuano dhidi ya Barrack Y.C.II ya Liberia
ambayo katika raundi ya awali iliitoa Johansens ya Sierra Leone. Barrack
ilishinda bao 1-0 nyumbani katika mechi ya kwanza na kulazimisha suluhu
katika mechi ya marudiano jijini Freetown.
Azam
itaanzia mechi hiyo ugenini kati ya Machi 15,16 na 17 mwaka huu wakati
mechi ya marudiano itachezwa Tanzania kati ya Aprili 5,6 na 7 mwaka huu.
0 Comments