Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall' uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali (picha na Freddy Maro)
WATENDAJI KITUO CHA UOKOZI MWANZA WATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA DHARURA KWA SAA
24
-
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo
cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza, chenye thamani ya
takriba...
26 minutes ago





0 Comments