Na Elizabeth
John
TAMASHA
la Pasaka mwaka huu linatarajiwa kufanyika kwa siku nane mfululizo kuanzia
Machi 31 hadi Aprili 7 katika mkoa saba, ikiwa ni mara ya kwanza tamasha hilo
kufanyika mikoa zaidi ya mitatu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo la kimataifa, Alex
Msama, wamefanya hivyo kwa kuheshimu maoni ya wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki
wa injili, ambao kwa kuguswa na tamasha hilo, wameomba kufikiwa ili kuzoa
baraka za Mungu ambazo huambatana na ujumbe wa nyimbo mbalimbali kutoka kwa waimbaji
wa ndani na nje ya Tanzania.
Msama
alisema kuwa, maadamu kamati yake imeridhia maombi ya kuongeza idadi ya mikoa,
wanawasihi wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa injili katika mikoa ambayo
Tamsha litafika, kujitokeza kwa wingi kujionea na kuchota baraka za Mungu
kupitia ujumbe wa nyimbo na hakuna atakayejutia muda wake wa kwenda
kulishuhudia.
Mikoa
rasmi iliyoshinda katika kivumbi cha uwenyeji wa tamasha hilo ni Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza na Mara, ambayo imepatikana baada ya wapenzi,
mashabiki na wadau kupiga kura kwa njia ya simu na kilichobaki sasa ni Kamati
ya maandalizi kutimiza ahadi yake ya kuwapelekea uhondo huo wa muziki wa
injili.
Msama
alifafanua kuwa, baada ya Tamasha hilo
kuzinduliwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Machi 31, siku itakayofuata litakuwa
Uwanja wa Sokoine Mbeya kabla ya kutua Uwanja wa Samora, Iringa Aprili 3 na
Aprili 6, itakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma na siku itakayofuata kishindo
cha tamasha hilo
kitatua CCM Kirumba, jijini Mwanza.
0 Comments