Mwigiizaji
maarufu Nadhipa ameanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro leo asubuhi
akiwa na wanawake wengine 10 kwa ajili ya kuhamasisha ukatili dhidi ya
wanawake.
Katika msafara huo wapo
Watanzania Wawili, Ashura Kayupayupa, ambaye ni mwanaharakati dhidi ya ndoa za
mapema na Mwalimu Anna Philipo ambaye ni Mwanaharakati dhidi ya unyanyasaji wa
kijinsia kutoka katika jamii ya Wahadzabe.
Kutoka Nepal ni Shailee
Basnet, Pujan Acharya, Nimdoma Sherpa, Pema Diki Sherpa, Chunu Shretha, Asha
Kumari Singh na Maya Gurang, pamoja na wapiga picha wawili James Gimbrone na
Russ Paraseau
0 Comments