MSTAAFU WA IKULU AVUNJIWA NYUMBA YAKE




TINGATINGA likivunja nyumba iliyopo mtaa wa Ohayo kitalu namba 15 iliyokuwa inamilikiwa na Kapteni Msataafu wa Ndege ya Rais Felix Kileo Chini ya Kampuni ya udalali ya Rhino Auctionmart, kwa madai kuwa kampuni hiyo imepewa kazi hiyo ya kubomoa na tassisi ya Benki ya Wakulima TIB. Kwamujibu wa maelezo ya wabomoaji hao TIB wanataka kujenga jengo la ghorofa kwenye eneo hilo, baada ya nyumba hiyo kupewa na serikali na mtumishi wa serikali aliyekuwa anaishi kwenye nyumba hiyo kupewa nyumba nyingine lakini alikaidi kutoka ndio maana kampuni hiyo imeingia kwa kuvamia nakuanza kuvunja.
Tingatinga likivunja sehemu ya nyuma ya nyumba hiyo.
Kazi ya kubomoa jengo hilo ikiendelea chini ya usimamizi wa Kampuni ya Udalali ya Rhino Auctionmart.
Kutokana na kuta za nyumba hiyo kuwa ngumu kazi ya ubomoaji ililazimika kuanzia madirishani ili kurahisisha ubomoaji.
Nyumba hiyo ikiondolewa milango mapema kabla haijaanza kuvunjwa.

ALIYEKUWA Rubani wa ndege ya Rais kwa awamu zote nchini Kapteni Felix Kileo, leo ameondolewa kwa nguvu ndani ya nyumbayake na kubomolewa na Kampuni ya Udalali ya Rhino Auctionmart, huku kukiwa na madai ya kuwepo kesi mahakamani inayoendelea.

Kwamujibu wa wabomoaji hao wanadai kuwa wamepata idhini ya kubomoa nyumba hiyo kutoka kwa Taasisi ya Benki ya Wakulima (TIB) ambayo inakusudia kujenga Ghorofa kwenye eneo la nyumba hiyo lililopo mtaa wa Ohayyo kitalu namba 15.

Ndugu wakaribu wa Kapteni huyo ambae mwenyewe hakuwepo kwa muda huo eneo la tukio wamelalamikia kitendo anachofanyiwa nduguyao hasa ukizingatia ni mtumishi wa siku nyingi wa serikali.

“Huyu mimi ni nduguyangu amekuwa mtumishi wa serikali za awamu zote amestaafu mwaka jana kama rubani wa ndege ya Rais lakini anachofanyiwa ni udhalilishaji, na vitendo hivi si vya kistaraabu hata kidogo ni ufisadi tu huu, pesa zitatoa roho ya mtu hi!” alisikika mmoja wa kaka wa Kapteni huyo.

Kwamujibu wa ndugu hao kesi ya msingi iko mahakamani na keshokutwa inasikilizwa lakini wameshangazwa kitendo cha kuwavamia bila hata barua ya mahakama na kuvunja nyumba hiyo.

Taarifa ilizozipata blog hii kutoka eneo la tukio nikwamba mtumishi huyo wa Serikali alitakiwa kuhama kwenye nyumba hiyo ili kupisha ujenzi wa jingo la Benki hiyo nayeye kupewa nyumba nyingine yakuishi lakini alikataa na upande wa Serikali kufungua kesi.

Baada ya kufunguliwa kesi upande wa serikali ulishinda lakini Kapteni huyo kupitia mawakiliwake walikata rufaa iliyosabisha zoezila kuendeleza kiwanja hicho kusimama.Chanzo : NdgShilatu Blog.

Post a Comment

0 Comments