Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamalle (Kulia) akisisitiza jambo kwenye mwendelezo wa vikao vya maandalizi ya kampeni ya kulipamba taifa na Sanaa za nyumbani vinavyofanyika Ukumbi wa BASATA. Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego na Katibu wa shirikisho hilo Godfrey Ndimbo.
NaMwandishi Wetu
Wadau mbalimbalinchini hususani viongozi wa kitaifa na kidini, wanasiasa na wamiliki wa majengombalimbali nchini wameombwa kuunga mkono kampeni ya kulipamba taifa na kazi zaSanaa za kitanzaia inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Akizungumza katikatiya wiki hii kwenye mwendelezo wa vikao vya maandalizi ya kampeni hiyo Rais waShirikisho la Sanaa za Ufundi nchini Adrian Nyangamalle alisema kuwa uungwajimkono wa wadau hao utalifanya taifa kupendeza na kuwa kivutio kwa kila mtu.
“Tunategemea kwa kiwango kikubwa uungwaji mkono kutoka kwa wadau hasa viongozi wetu wa kitaifa,lengo ni kumfanya kila mtanzania aone fahari kwa kupamba na Sanaa za nyumbani lakinipia afurahie mandhari nzuri ya taifa lake” alisema Nyangamalle.
Kwa mujibu waNyangamalle, Tanzania imejaaliwa Sanaa nyingi za mikono kama za vinyago na michoro,zina mvuto wa aina yake, zinavuta wageni wengi kuja kuzitazama hivyo kuzipambakwenye maeneo yetu ya wazi na maofisi kutabadili kabisa muonekano wa miji naofisi zetu.
“Tunalenga kampenihii isambae, ifike mahali iwe lazima kwa ofisi zetu za umma na maeneo ya wazi kupambwana Sanaa za mikono kutoka nyumbani. Ni wazi viongozi wetu wakiunga mkonotutaleta mabadiliko” alisisitiza Nyangamalle.
Kuhusu mikakati yauzinduzi wa kampeni hiyo Rais huyo mwenye dhamana na Sanaa za mikono nchinialisema kuwa, inaendelea vizuri na kwa hatua za mwanzo itahusisha maonesho yaSanaa za kupamba maofisini sambamba na kushawishi watendaji maofisini kununuakazi hizo za mikono.
“Bado hatujapangakalenda rasmi ya uzinduzi wa kampeni hii lakini mikakati inaendelea vizuri,wito wangu ni kuomba viongozi wetu wa juu na watanzania kuona umuhimu wakampeni hii” alimalizia Nyangamalle.
0 Comments