UKWELI KUHUSU UTATA WA UMRI WA LULU MAHAKAMANI KUU KESHO

LULU AKISINDIKIZWA NA ASKARI MAGEREZA.

KESI ya mwigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' itaotolewa uamuzi wake kesho katika Mahakama Kuu saa tatu asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Hiyo ni kwa mujibu wa Jaji Dk. Fauz Twaib aliyesikiliza  kesi hiyo iliyofikishwa Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam kwa shauri la ufafanuzi juu ya umri  wa mshtakiwa.

Jaji  Twaib huyo alidai Mahakamani hapo wiki mbili zilizopita  kuwa kutokana na utetezi kuwa mrefu hivyo hana budi wa kupata muda ili aweze kuupitia  na uamuzi wake utatolewa   Juni 11 (Kesho)  katika  Mahakamani hiyo.

Aidha mawakili wane ambao wanamtetea  Lulu waliiomba Mahakama hiyo kuchunguza umri wa Lulu au watoe idhini kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuchunguza.

Hadi sasa Lulu anatetewa na Mawakili  wanne ambao ni Jacqueline Dimelo,Kennedy Fungamtama, Fulgency Massawe na  Maico Kibatala.

Huku Mawakili kwa upande wa Serikali ni Shadrack Kimaro na Elizabeth Kaganda.

Lulu anakabiliwa na tuhuma za kifo cha aliyekuwa mcheza filamu nyota nchini Steven Charles Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake Sinza Vatican Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments