SHUKRANI KWA SERIKALI KUSIKIA KILIO CHA WASANII.

WILSON MAKUBI
KATIBU MTENDAJI LA FILAMU TANZANIA – TAFF.
 Mheshimiwa Rais,kwa niaba ya Bodi,Kamati kuu,wanachama na wadau wa  Shirikisho la Filamu Tanzania,TAFF, napenda ufahamu kwamba Shirikisho ni taasisi inayoundwa na muungano wa vyama vinavyojihusisha na kazi za utayarishaji wa filamu nchini, ambalo lilianzishwa kwa tamko la serikali mwaka 2009 na kusajiliwa mwaka 2010 kwa sheria namba 23 ya mwaka 1984 lakini pia inatekeleza majukumu yake kwa kupitia sheria namba 4 ya mawaka 1976 ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kanuni zake.

Mheshimiwa Rais, Vyama vinavyounda Shirikisho hili ni Chama Cha Waigizaji, Chama Cha Waongozaji, Chama Cha Watayarishaji, Chama Cha Wasambazaji,Chama Cha Wahariri, Chama Cha Watafuta mandhari , Chama cha Watunzi na chama cha Wapiga picha za filamu, vyama vyote vimesajiliwa na kutambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kwa kipindi kirefu sana tasnia ya filamu na sekta ya sanaa kwa ujumla imekuwa katika mazingira hatarishi kwa mustakabali wa maslahi ya wasanii wenyewe. Lakini tatizo hili lilisababishwa na
a.    mtazamo hasi ambao ulianzia katika misingi mikuu ya sheria
    kuifanya sanaa kuwa ni kiburudisho na
b.    mfumo mbaya wa biashara ya sanaa ambapo bei haipangwi na
    mtayarishaji bali hupangwa na mnunuzi.(Mfumo huu umesa
         babisha kutowepo kwa takwimu sahihi za mapato yanayotokana
         na shughuli za tasnia ya filamu na filamu zenye ubora
         viwango vya soko la kimataifa )   
jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa sanaa ya Tanzania kudumaa,kuwa watumwa katika kazi zao na wasanii kutokuwa na maslahi stahiki yanayotokana na kazi zao.

Kuanzia mwa mwaka 2005 tasnia ya filamu hapa nchini ilianza kupata sura ya kibiashara zaidi, ambapo Wasanii wa filamu na muziki walianza kuona matunda yanayotokana na kazi zao japo kidogo, ingawa bado kuna tatizo la malipo madogo yasiyokidhi na kuakisi gharama halisi za uzalishaji wa filamu.

Mheshimiwa Rais kwa kipindi chote ambacho filamu na muziki wa Tanzania ukiwa ni mkombozi wa ajira kwa vijana wengi lakini bado tatizo la wizi wa kazi hizo unaendelea kufanyika tena kwa kiwango cha juu sana kiasi cha kuathiri mauzo ya kazi hizo.Wasanii kupitia Shirikisho lao walipiga kelele sana ili kulinda hadhi ya kazi zao, haki ya ubunifu wao na maslahi ya kazi zao.
 Pamoja na kilio hicho cha muda mrefu wasanii hawakuacha kufanya kazi katika mazingira yopte hayo wakiamini suala kudai kupigania haki ipo siku litapatiwa ufumbuzi na serikali yao makini.
Kwa Mmantiki hiyo tunakushukuru wewe binafsi na serikali yako pia kwa kuchukua hatua za makusudi katika kulishughulikia jambo hili.
     Shirikisho la Filamu Tanzania linapongeza hatua zilizochukuliwa  katika kurasimisha tasnia ya filamu na muziki Tanzania ili kuondoa tatizo la wasanii kutonufaika na jasho la kazi zao.
Hatua za kutafuta ufumbuzi endelevu wa tatizo hili zimeanza muda mrefu ambapo awali iliundwa kamati ya pamoja kati ya Shirikisho la Filamu , Muziki na TRA.Lakini pia katika kuhitimisha mawazo ya kupata namna sahihi ya kuondoa kero hii ilihitimishwa na kikao kati ya Mheshimiwa Waziri wa Habri Vijana na Utamaduni na Wasanii wenyewe kilchofanyika mwezi Mei 2011.
     Tunaipongeza Serikali kwa kupitisha matumizi ya stampu ya TRA kama wasanii wenyewe walivyoomba ambazo zitakuwa na alama za usalama (security features )na Barcode katika kazi za filamu na Muziki. Tunaamini kwamba urasimishaji huu utasaidia kuifanya kazi hii kuwa ni yenye heshima na itayoweza kukopesheka kama ilivyo kwa wafanyabiashara wadogo wa chakula maarufu kama mama lishe!.
      Lakini pia mfumo wa kielectronic utaotumika utarahisisha uwekaji na upatakaji wa taarifa, usimamizi wa mauzo, uangalizi wa mapato na namna tasnia ya filamu inavyoendeshwa.

Ushauri/Ombi letu.
     Mheshimiwa Rais,katika kurahisisha wadau wa filamu kukopeshwa tunashauri Serikali itoe tamko katika taasisi za fedha kutambua hati maalumu ya utambulisho kutoka shirikisho la Filamu Tanzania (Certificate of Recognition)  ikiwa ni ambatanisho la ziada kwa muombaji ambaye ni msanii wa fani ya filamu.  
Serikali kupitia vyombo vyake vya sheria na mamlaka husika wasimamie utekelezaji huu kwa vitendo mara utapoanza.

Mwisho tunaomba upokee shukrani zetu pia tunakutakia kazi njema katika ujenzi wa taifa.

Post a Comment

0 Comments