Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego akisisitiza jambo wakati akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA.Wengine kulia ni Mhandishi Joel Chacha kutoka malaka ya mawasiliano nchini (Tcra) na Kaimu Mratibu wa Jukwaa hilo Agnes Kimwaga.
Bw. Joel Chacha kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii iliyohusu Teknolojia ya Digital na Faida Zake Katika Sekta ya Sanaa na Wasanii.Kulia ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego.
Mdau kutoka Mlimani TV akiuliza maswali kuhusu mfumo wa Digitali Mmoja wa Wasanii aliyehudhuria mjadala huo akitoa ya moyoni kuhusu mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda ule wa Digitali na mchango wake kwenye Sanaa.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria mjadala huo wakifuatilia kwa makini elimu iliyokuwa inatolewa.
Baraza la Sanaa laTaifa (BASATA) limewataka wasanii kujipanga kwa ajili ya kuhimili ushindani wakimataifa kutokana na ujio wa mfumo wa digitali ambao utazifanya kazi zaokuonekana kimataifa.
Wito huo umetolewawiki hii kwenye ukumbi wa BASATA na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, GhoncheMaterego wakati akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa uliohusu Teknolojiaya Digital na Faida Zake Katika Sekta ya Sanaa uliochokozwa na MhandisiJoel Chacha kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Alisema kuwa, mfumowa digitali utaruhusu uwepo wa vituo vingi vya redio na runinga ambavyovitakuwa na masafa ya kimataifa hivyo ni wazi wasanii wanatakiwa kujipangakatika kuandaa maudhui bora, ya kutosha na yenye mvuto kwa ajili ya kukidhiongezeko hilo na zaidi ushindani wa kimataifa.
“Wasanii tujipange,fursa zinazokuja ni nyingi mno, zinahitaji maudhui ya kutosha, yenye ubora nayatakayoweza kuvifanya vyombo vya habari viweze kuhimili ushindani pia”alisisitiza Materego.
Aliongeza kuwa,moja ya eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wamiliki wa vyombo vya habari niuhafifu wa maudhui ya kazi za Sanaa hivyo, wasanii hawana budi kuachakulalamika na kujipanga kukabili changamoto hiyo.
Awali akiwasilishamada hiyo,Mhandisi Chacha alisema kuwa, mfumo wa digitali utazalisha fursanyingi katika sekta ya Sanaa lakini akasisitiza kuwa, uchangamfu wa Wasaniiwetu ndiyo utawafanya wafaidi.
Alizitaja baadhi yafursa hizo kuwa ni pamoja na; ongezeko la ajira kwa Wasanii, ongezeko lavipindi, kukua kwa ushindani katika ubunifu na utengenezaji maudhui yenyeubora, Sanaa za Tanzania kutangazika kimataifa na kuongezeka kwa makampuniyatakayojihusisha na sekta ya Sanaa
“Mfumo wa digitaliuna mazuri mengi lakini kubwa ni kuongezeka ushindani na ubora katikakutengeneza maudhui yenye ubora na pia ongezeko la masafa katika televisheniambayo yatahitaji maudhui (vipindi) ya kutosha” Aliongeza Chacha.
Hata hivyo,aliitaja changamoto ya uharamia kwenye sekta ya Sanaa ambapo aliwashaiuriwasanii kuamka na kujiunga na Chama cha hakimiliki (Cosota) ili kuhakikishakazi zao zinalindwa kisheria.
Wadau wengiwaliochangia mjadala huo walionekana kuwa na wasiwasi na mfumo wa digitalilakini wakaomba elimu ya kutosha itolewe ili wananchi wengi zaidi waelewe ninimaana ya kutoka mfumo wa analogia kwenga ule wa digitali.
0 Comments