WABUNIFU WA MITINDO WAJIFUNZA MENGI AFRIKA KUSINI


                                                                  Millen Happiness Magesse.
JohannesburgAfrika Kusini  
WABUNIFU wannewa mavazi walioshiriki wiki ya mitindo Afrika Kusini wameeleza kufurahishwakwao na ushiriki wao huo huku wakifafanua yale waliyojifunza wakiwa nchinihumo.

Ziara hiyoiliyodhaminiwa na mwanamitindo mahiri Millen Magese inalenga kukuza nakutangaza tasnia ya ubunifu wa mavazi na uanamitindo wa Tanzania  katika anga la kimataifa kupitia mradi waTanzania International Fashion Expose (TIFEX).

Wakizungumzakatika nyakati tofauti wabunifu hao walifafanua kuwa onesho hilo limewafundishamengi kwa kuwa wamekutana na wabunifu kutoka nchi mbalimbali za ndani na nje yabara la Afrika.

Mbunifu EvelynRugemalira alisema kuwa ameweza kujifunza namna ambavyo wabunifu wa njewanavyojitangaza na kutafuta soko.

Nayembunifu   Doreen Noni kupitia lebo yake ya Eskado Bird alisemakuwa  mara nyingi amekuwa akishirikikatika maonesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, mwaka huu ametengeneza nguoza kuvutia zaidi

Alisema kuwakupitia onesho la wiki ya mitindo hapa Afrika Kusini ameshajipatia soko lakimataifa kwa kuwa onesho hilo limemtangaza zaidi.

Naye JamiraVera Swai akishirikiana na Julie Lawrence alisema kuwa kupitia tamasha hilinguo zake zitatambulika kimataifa zaidi na kuweza kumweka katika ramani yaAfrika. Julie kupitia mradi wake wa fahari uliopo kisiwani Zanzibaraliwavalisha vidani na mikoba wanamitindo waliovaa nguo za Jamila.

Naye mratibuwa ziara hiyo Millen Magese alisema kuwa  “Nimefurahi sana kufanikisha ziara hii kwanimwanzo wa kutangaza kazi zetu kimataifa umeanza vizuri kupitia fani hii ya wabunifuwa mavazi na wanamitindo, nawaamini watanzania na vipaji vyao na ninatumaini yakuwa watatambua mradi huu ni kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments