WAKATI shughuli za maziko ya Kanumba zikielezwa kumalizika,kamati iliyokuwa ikishughulikia hilo hajakabidhi michango iliyotolewa na watu mbalimbali katika kipindi chote cha msiba.
Mmoja wa wanafamilia aliliambia Sayari kwamba cha kushangaza zaidi tangu juzi walipokuwa wakiwapigia simu wajumbe wa kamati hiyo kila mmoja kwa nyakati tofauti hawakupokea huku wengine wakizima simu zao kutwa nzima.
Kama vile haitoshi ndugu huyo alisema baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wameshaanza kutoa taarifa kwa familia kuwa kuna uchakuachauji unataka kufanywa na kamati hiyo na ndio maana kumekuwepo na ukimya huo.
‘Hili jambo linaonekana limeshafika mahali pabaya na hawa wajumbe watakuwa wamezidiana kete ndio maana wameamua kuanza kutoleana siri,hebu ngoja tuone mwisho wake utakavyokuwa”alisema mwanafamilia huyo
Kutokana na taarifa hizo mwandishi wa habari hizi alifanya juhudi za kumtafuta Mwenyekiti wa kamati hiyo,Gabriel Mtitu,ambaye simu yake iliita muda mrefu bila ya kupokelewa.
CHANZO GAZETI LA SAYARI
0 Comments