FILAMU ALIYOTABIRI KIFO CHAKE YAKANUSHWA NA MUHUSIKA MKUU

WAKATI kukiwepo na taarifa ya kwamba Kanumba alitabiri kifo chake kupitia filamu yake ya ‘Power and Love’ ambayo ilikuwa katika hatua za uhariri,aliyeigiza naye kama mke wake katika filamu hiyo,Irene Paul, amesema maneno hayo hayana ukweli wowote.

Irene alisema kutokana na uzushi huo alilazimika kumpigia simu anayeyaeneza taarifa hizo na kumueleza kwamba amuache marehemu apumzike kwa amani na kuepuka kutumia jina lake kupata umaarufu.
‘Jamani mimi ndiye niliyecheza kipande cha mpenzi wa Kanumba ambaye nilimsaliti baada ya kunipatia figo yake moja.

“Filamu hiyo inaelezea namna Kanumba alivyoweza kunipatia figo hiyo baada ya mimi kupata tatizo la figo na alikuwa akifanya hivyo kwa kuwa alinipenda sana.

Lakini wakati huohuo mimi nilikuwa na mpenzi wangu mwingine tajiri ambaye ni Patcho Mwamba aliyenikimbia baada ya kuona nimepatwa na matatizo.

Mwisho wa siku ninapona nagundua kuwa nahitaji msaada mwingine wa kulipiwa kodi ambapo ninapomwarifu Kanumba yeye ananijibu kuwa hana fedha kwa wakati ule kwa kuwa naye alikuwa katoka kulipia kodi ya nyumba anamoishi na sitoshe alikuwa masikini.

Majibu hayo yananifanya nirudiane na mpenzi wangu wa awali huku nikimpa maneno ya kejeli Kanumba kuwa siwezi kuwa na mwanaume suruali na pale anaponishika ili kunielewesha mapenzi aliyo nayo juu yangu namsukuma na kudondokea kwenye kiti kisha mimi naondoka zangu na kumuacha pale.

Sehemu hiyo ndio inatafsiriwa vibaya na huyo mtoa habari kwamba alidondoka chini na kupoteza maisha ambapo Daktari aliyehakikisha kupoteza maisha ndio huyo aliyefanya hivyo siku ya kufa kwake.

Napenda kuwahakikishia watanzania hakuna kitu kama hicho,na ukweli wa hili ninaloliongea watakuja kuliona pindi filamu itakapotoka labda tu waamue kubadilisha kwa makusudi kipande hicho na si vinginevyo.

Hata hivyo Irene alisema kitu ambacho kinamumuuma hadi leo kutokana na msiba huo ni pale Kanumba alipomuita wakati anaigiza kipande alichukuwa akimlalamikia mama yake kuwa ni kwa nini binadamu wamekuwa wepesi kusahau mema anayowafanyia kwa kuwa alimpenda sana mwanae na ndio maana aliamua kumtolea figo yake moja na kumuahidi kwamba pia yupo tayari kumpa roho yake kama atataka iwe hivyo ili kuonyesha upendo alionao juu yake.

Wakati anaigiza kipande hicho ambacho hata hivyo kinaelezwa Kanumba alimau kukiingiza ghala kwa kuwa hakikuwepo kwenye script tangu awali, Irene alisema alimuita peke yake amuangalie jambo ambalo lilimtoa machozi pindi alipokuwa akimwangalia anaigiza.

Alisema mpaka sasa anajiuliza ni kwa nini Kanumba aliamua kumuita wakati hata alikuwa hausiki katika kipande hicho kwani mara nyingi katika filamu kama huusiki hautakiwi kuwepo hapo.

Post a Comment

0 Comments