Nd. Fabian Kulwa pamoja na watoto Emmanuel ( Gulu), Josephine, George, Nicodemus ( Kifunta) na Pauline ( Shafa) tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wote walioshirikiana nasi katika kumuuguza na hata katika msiba mzito wa mama yetu mpendwa Joyce Kulwa.
Shukrani za dhati ziwafikie madaktari na wauguzi wa Kwamndolwa Missionary Hospital- Korogwe, Regency Medical Centre na Hospitali ya Muhimbili kwa huduma zao nzuri na jitihada zao za kuokoa maisha ya mama Joyce Kulwa.
Vile vile tunapenda kuwashukuru wote wanaohusiana na ukoo wa Masayanyika na Kulwa kwa ushiriki wao wa dhati katika kumuuguza na hata katika msiba na maandalizi ya mazishi kwa Dar es Salaam na Korogwe- Tanga.
Shukrani pia zimfikie Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Maafisa wake waandamizi na familia zao kwa jinsi walivyoguswa na kuugua na hata msiba huu. Halikadhalika, tunaushukuru Uongozi na Wafanyakazi wa NMB, TAZAMA Pipelines na Chuo cha Usafirishaji kwa kuwa karibu nasi wakati wote.
Shukrani za kipekee zimuendee Askofu na Uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Katibu Mkuu na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mkuu wa jimbo la Tambarare- Korogwe, Uongozi wa KKKT Usharika wa Mwenge, Kijitonyama- DSM , Baba Paroko, Masista na Waumini wa Parokia ya Mt. Martha ya Mikocheni- DSM, Baba Paroko na Waumini wa Parokia ya Mt. Augustino- Korogwe, Wazee wa Kanisa na Waumini wa KKKT Usharika wa Korogwe, Makundi mbalimbali ya wanamaombi na watu binafsi waliotoa huduma za kiroho na kutufariji katika kipindi chote hiki.
Tunamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na Familia yake, Waheshimiwa Wabunge wa Korogwe Mjini na Mlalo, Viongozi na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Walimu na wanafunzi wa Oysterbay kwa miaka ya 1980 na 1990, Vikundi mbalimbali vya Kanisani na Kijamii ambavyo Marehemu alikuwa anaviongoza au kushirikiana navyo , Ndugu, Jamaa, Majirani na Marafiki wa Dar es Salaam na Korogwe kwa misaada yao ya hali na mali pamoja na faraja kuu katika kipindi chote hiki.
Tunaomba wote kwa ujumla mpokee shukrani zetu za dhati. Arobaini ya Mama Joyce Kulwa itakuwa Tarehe 8 Aprili 2012 ambapo kutakuwa na Sadaka ya Shukrani ya Maisha yake. Mkesha utakuwa Tarehe 7 Aprili 2012 nyumbani Korogwe. Wote mnakaribishwa.

0 Comments