Mawakala wa Redd's Miss Tanzania katika picha ya pamoja.
MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wa shindano la urembo nchini, Hashim Lundenga, amesema kwamba, kampuni yake mwaka huu itahakikisha inatafuta mwakilishi mwenye upeo katika kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Tanzania 2012.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaa na Lundenga, katika semina ya mawakala wanaoandaa Redd’s Miss Tanzania 2012.
“Katika mashindano ya mwaka huu tunahitaji mrembo ambaye atakuwa na upeo wa kutosha, hasa wa kujibu maswali ikiwa ni sambamba na ubongo wake kuwa safi siyo wauza sura. Huu ni mkakati maalum wa Kamati yetu, ili kufanya vema katika mshindano ya dunia” alisema Lundenga.
Katika semina hiyo ya siku mbili, mawakala hao waliweza kujifunza madhumuni, kanuni, sheria na taratibu za mashindano, sifa za washiriki, wajibu wa washiriki, wajibu wa mawakala, miiko ya uongozi, zawadi za washindi na washiriki.
Kutoka kulia ni Mratibu wa Miss Kigamboni City Somoe Ng'itu, Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania Albert Makoye, Mkurugenzi wa Miss Kigamboni Mamaa Angela Msangi na Asela Magaka muandaaji wa Miss Shinyanga hapa wakiwa katika hoteli ya Giraffe View katika semina ya siku mbili jana na leo ya Redd's Miss Tanzania.
Mwendeshaji wa Blog ya http://www.mromroki.blogspot.com/ almaarufu kwa jina la Father Kidevu pia ndiyo Mpiga picha wa Redd's Miss Tanzania akiwajibika.
Mimi na Asela Magaka ambaye ni mwandaaji wa Miss Shinyanga ambapo amekuwa akitoa warembo bomba mara kadhaa huku wakifanikiwa kuingia katika ngazi ya Taifa.
Mama Salome Kiwaya Kulia ambaye ni mdau wa urembo wa muda mrefu nchini pia ni Mratibu wa Miss Dodoma Kanda ya Kati tangu mwaka 1994 hadi sasa pia ni mmiliki wa bendi ya SAKI STARS ka wale wenyeji wa Mkoa wa Dodoma wanalifahamu hilo.
Wandaaji wa urembo kutoka Kanda ya Ziwa katika picha ya pamoja.
0 Comments