Kulia ni Msanii Cleopas Tlou Monyepao 'DJ Cleo' na Thabo Lephaneane DJ Soul T wakizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO Dar es Salaam.
Kutoka Kulia ni Mtaribu na Msemaji Yvone Moyo, Cleopas Tlou Monyepao 'DJ Cleo' na Thabo Lephaneane DJ Soul T na Msanii wa hapa nchini Ommy Dimpoz.
YULE msanii na machachari Tlou Monyepao ‘DJ Cleo’ kutoka nchini Afrika kusini ametoa wito kwa wapenzi wake kujitokeza kwa wingi katika onesho lake lililopangwa kufanyika usiku wa leo katika viwanja vya Posta vilivyopo maeneo ya Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
DJ Cleo ambaye amejizolea umaarufu kwa kupitia kibao chake cha ‘Face Book’ ameahidi kufanya mambo makubwa katika onesho lake la pili baada ya kufanya onesho lake la kwanza lililopangwa kufanyika usiku wa leo ukumbi wa Club Much More usiku wa jana uliopo ndani ya Club maarufu nchini Club Bilicanas .
Cleo anakiri kwamba yeye ni bonge la msanii mbali ya kuwa DJ na kazi hiyo aliianza siku nyingi na anafurahishwa na jinsi alivyojizolea mashabiki pia alizitaja nyimbo zake zingine mbali ya ‘Face Book’ ni pamoja na ‘Wena ng' Hamba Nawe’, ‘Akulalwa’, ‘Mind ckuf’.
DJ Cleo aliyasema hayo jana wakati alipozungumza leo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, Dar es Salaam.
Akiizungumzia kama anaifahamu nchi ya Tanzania na wasanii wake kwa ujumla alisema kuwa nchi zote zina uhusiano mkubwa ambapo nchi hizi zinaingilia kwa mambo mengi huku akigusia suala la mahusiano mema ya kisiasa, kiuchumi na hata kifamilia kwa ujumla.
DJ Cleo anakiri kwamba yeye ni msanii na huku akisema kwamba anafurahi kuona kwamba ngoma yake ya FaceBook inabamba na kwamba anazo zingine nyingi tu zaidi ya hiyo.
Onesho hilo limeratibiwa na Kituo cha redio cha Times FM na msemaji wake akiwa ni Yvone Moyo ambaye alisema mbali ya DJ Cleo wasanii kadhaa wa hapa nyumbani watatumbuiza.
Moyo anawataja wasanii hao kuwa ni kutoka katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya ambao ni pamoja na Ommy Dimplez, Suma Lee , Tip Top Connection Dully Sykes, Linex, Juma Nature (na Wanaume Halisi), Chegge & Temba (Wanaume Family). Kiingilio ni sh. 10,000.
0 Comments