WANAMUZIKI NA BONGO MOVIE KUCHANGIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

TIMU ya Soka ya wachekeshaji na waigizaji (Bongo Movies) keshokutwa inatarajiwa kumenyana na wanamuziki wa muziki wa dansi, mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa mafuriko yaliyolikumba jijini la Dar es Salaam hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compact Media, Eliya Mjatta, alisema, wameandaa mchezo huo ikiwa ni sehemu ya kampeni yao waliyoianzisha na kuipa jina la ‘tuwasaidie wahanga wa mafuriko Dar es Salaam baada ya kuguswa na matatizo yaliyowakuta watanzania wenzao.
Alisema, licha ya mchezo huo kutakuwa burudani kutoka kwa wasanii, wachekeshaji na wanamuziki hao wakiunda bendi moja kabla mechi hiyo itakayowaburudisha maelfu ya wananchi watakaojitokeza uwanjani hapo.
Mjatta alisema, mlezi wa timu ya wachekeshaji ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki na kwa upande wa wanamuziki ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambako kiingilio kitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na maeneo mengine shilingi shilingi 2,000.

Alisema, kabla ya mchezo huo leo wanatarajiwa kwenda Mabwe Pande, ambako baadhi ya waathirikika hao wamehamishiwa kujionea matatizo yanayowakabili ili fedha watakazikusanya wajue namna ya kuzielekeza kwenye tatizo husika.

Post a Comment

0 Comments