Asha Baraka kushoto akiwa na aliyekuwa Rais wa bendi ya Mashujaa Jado FFU, ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo siku chache kabla mwanamuziki Chalz Baba hajatwaliwa na bendi hiyo kutoka bendi konge ya muziki nchini The African Stars 'Twanga Pepeta' ambayo hapo awali ilifahamika kama Chipolopolo baadaye ikawa chini ya kiongozi Elyston Angai ambapo ilikuwa ikimilikiwa na Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET).
Kalili kulia na Jado FFU
Hapa ilikuwa ni katika viwanja wa Leaders Club ambapo Asha alitinga muda mfupi tu baada ya kuambiwa mahasimu wake bendi ya Mashujaa wanafanya onyesho huku wakiwa wameparamia jukwaa lililotengenezwa na ASET.
Hivyo basi mara baada ya kusikia hivyo ndipo mama huyo alipokanyaga mafuta hadi Leaders Club kwenda kuwadai wamlipe kiasi cha sh.100,000 kama tozo ya kutumia jukwaa.
"Chacha njoo wewe ndiyo Meneja wa Leaders na unajua taratibu zote hivyo ukitaka tuelewane washushe wakapigie wkingine la sivyo wanilipe sh.100,000 yangu ya kutumia jukwaa, hizi ni dharau bwana mimi sitaki wanipe changu mwanamuziki wangu waniibie dukani kwangu wamekuja kutukana sasa nini vinginevyo nalianzisha" alisema Asha bila kuonesha chembe ya utani.
Muda ulipita huku Meneja wa Leaders akihaha kutafuta suluhu kwa kujitetea kwamba anajua utaratibu huo hivyo aliomba Asaha amsamehe kwa siku hiyo lakini Asha alisema yeye yuko kibiashara zaidi hivyo apewe chake ndipo aotaondoka katika viwanja hivyo.
"Tusileteane dharau katika biashara ninyi si mnahela sana tengenezeni jukwaa lenu mtumie kwwa nafasi hili mimi mwenyewewe nimelichomelea na kushinda hapa na mafundi hakuna dezo hapa mjini leteni changu niondoke"
Wakati hayo yakiendelea Bongoweekend ilikuwepo katika eneo la tukio na kushuhudia Meneja wa bendi ya Mashujaa aliyetambulika kwa jina la Hamisi akihaha huku na kule kumtafuta mmoja wa wamiliki wa bendi Papaa Yohana Ndugu yake na hela aje amtoe Asha kwa kiasi hicho cha fedha.
Hamisi alisikika kila mara akisema Yohana hapokei simu sasa sijui itakuwaje jamani dada Asha sisi wote ni wa moja haya mambo yaache tu.
Lakini ghafla wadau waliokuwepo katika eneo hilo walimfuata Asha akawaeleza jinsi ilivyo huku Meneja wa Leaders Chacha akikubali kwamba jukwaa lile ni mali ya ASET na ni ruksa kutumiwa na bendi mbili tu ambazo ni Msondo Baba ya Muziki na Twanga.
Hivyo Hamisi aliamriwa atoe fedha hiyo na mara alikwenda sehemu ya mauzo na kurudi na pesa hiyo na mara alipotaka kumkabidhi Asha Baraka alizikataa na kumwamuru Chacha azichukue huku akisema atazifuata kwa muda wake lakini papohapo Chacha alizichukua zile fedha kutoka kwa Meneja wa bendi ya Mashujaa na kuziweka katika mfuko wa shati lake kisha akatoa pochi yake na kuhesabu kitita cha fedha na kumpa Asha akazipokea lakini alizigawa zote kwa wadau na kisha kuondoka katika eno hilo huku akiwataka wamiliki wa bendi kufuata taratibu na siyokufanya dharau katika mali za watu.
Lakini kabla Bongoweekend haijatokomea akatokea mdau mmoja na kuniuma sikio kwa kusema kuwa mmiliki wa bendi ya Mashujaa Maisha Hopaje a.k.a Papaa Maisha mara baada ya kupata habari hizo huku wengine wakidai alikuwepo katika eneo hilo lakini hakuonekana , alituma vijana wake walipime jukwaa hilo na kuahidi kuwa wanakwenda kutengeneza jukwaa lao.
Chalz Baba aliyekuwa Rapa na mwimbaji katika bendi ya Twanga Pepeta katikati akiwa katika sare za bendi ya Mashujaa ambayo amejiunga nayo hivi karibuni.
Chalz akizungumzia tifu hilo alisema kuwa "Mama yetu Asha hana matatizo bwana wampe chake aondoke anatulea sana huyu mama" Kadhalika na Jado FFU naye alisema hivyohivyo kama Chalz.
Kutoka Kulia ni Jado FFU , Asha Baraka na Rapa wa bendi ya Mashujaa Ibrahim a.k.a Mirinda Nyeusi ambaye ni Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakia wamepozi katika Viwanja vya Leaders Club hapa Asha akisubiria mkwanja wake.
0 Comments