Timu ya Taifa (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Novemba 3) kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 jijini N'Djamena. Wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini kesho, isipokuwa wale wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi ambao wataanza kuingia nchini Novemba 4 mwaka huu.
Kambi ya Taifa Stars itakuwa hoteli ya New Africa na mazoezi yatafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kulingana na programu za Kocha Mkuu wa timu hiyo Jan Poulsen. Timu inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 8 usiku kwenda N'Djamena.
Waamuzi wa mechi ambao wote wanatoka Nigeria ni Bunmi Ogunkolade, Tunde Abidoye, Baba Abel na Abubakar Ago. Mtathimini wa waamuzi atakuwa Idrissa Sarr kutoka Mauritania wakati Kamishna wa mchezo huo ni Hamid Haddadj (Algeria).
PRESS NOTICEShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho (Novemba 3, 2011) litakuwa na mikutano miwili na waandishi wa habari.
Mkutano wa kwanza Muda: saa 4.00 asubuhiMahali: TFF
Regards,
Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
Member, CECAFA Media Committee
0 Comments