Mdau Adam Mbogo akimvisha pete ya ndoa mke wake Matilda katika ndoa takatifu iliyofungwa katika Kanisa la Maxmillian Mwenge Jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita.
(Picha zote zimetumwa na Mdau http://www.jiachie.blogspot.com/ Michuzi Jr).
Wwooooowwww....! kwa raha zaoo maharusi wakilishana keki kwa staili ya kipekee kabisa. Blog ya JIACHIE inawatakia kila lakheri na fanaka tele katika maisha yenu mapya ya ndoa,Mungu akawabariki na kuwapa amani na upendo daima,bila kusahau uvumilivu kwa kila jambo na kumtanguliza Mungu siku zote za maisha yenu.
Maharusi wakiserubuka na wapambe wao pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya mnuso huo uliofanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Land Mark,Ubungo jijini Dar.
Maharusi wakiwa katika nyuso za furaha kabisa wakiwasalimia wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya mnuso wa harusi hiyo,iliyo fana kwa kiasi kikubwa,iliyofanyika kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Land Mark,Ubungo jijini Dar .
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wapambe waliokuwa maridadi kabisaa.Maharusi wakitoa sadaka kanisani mara baada ya kufunga ndoa mbele ya umati wa watu waliofika kulishuhudia tukio hilo adhimu na takatifu.
0 Comments