RAIS wa Shirikisho la Soka nchi (TFF),Leodgar Tenga ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuishangilia Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ katika mechi yake na Chad itakayochezwa Novemba 15 mwaka huu.Tenga aliyasema hayo jana ambapo Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao pia ndiyo wadhamini wakuu walipozkuwa wakizindua kampeni ya kuisapoti timu ya ‘Taifa Stars’ iweze kushinda.Tenga alisema Pambano hilo ni muhimu na wao viongozi wa TFF wako nyuma yao na tuna matumaini ya kushinda.
Akizungumza jana kwenye uzinduzi huo uliofanyika leo mchana katika viwanja vya wazi Karume Ilala Dar es asalaam alisema kampeni hiyo itafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam ambapo magari yatakuwa yakipita barabarani huku wakifanya promosheni ya Bia ya Serengeti na kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja katika bara na sehemu mbalimbali ambako kinywaji hicho kinapatikana.
“Wapenzi wa mpira tunawashukuru SBL kwa udhamini wao mkubwa ikiwa ni pamoja na kusimamia soka kwa nguvu zao zote kwani timu yetu iko vitano hivyo watanzania tuwaunge mkono katika kampeni hii ya ‘[Tuko pamoja tutashinda’” alisema Tenga.
Aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT), Dionese Malinzi alisema kwa niaba ya serikali naishkuru Kampuni ya Serengeti kutokana na udhamini wake kwa Taifa Stars lakini pia tunaomba waiangalie kudhamini na michezo mingine kama Gofu na mingineyo.“Hapa nchini kuna Kampuni nyingi lakini kampuni hii pekee imejikita zaidi katika soka hivyo nachukua fursa hii kuwaomba wamiliki wa Kampuni mbalimbali kujitokeza katika kutoa udhamini wa michezo kwani tunahitaji sapoti ya wapenda michezo” alisema Malinzi.

0 Comments